Pata taarifa kuu
CHINA-Maandamano-Siasa

Hong Kong: waandamanaji wajiondoa katika mazungumzo

Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu vya Hong Kong limetangaza kusitisha mazungumzo na Serikali. Waandamanaji hao wanaituhumu polisi kuwaruhusu baadhi ya watu kushambulia maeneo yao.

Ijumaa Oktoba 3, mji wa Hong Kong umeshuhudia machafuko, hususan mtaa huu wa Mongkok.
Ijumaa Oktoba 3, mji wa Hong Kong umeshuhudia machafuko, hususan mtaa huu wa Mongkok. REUTERS/Bobby Yip
Matangazo ya kibiashara

Ijumaa jioni wiki hii Hon Kong inakabiliwa na hali ya taharuki kati ya waandamanaji na polisi baada ya wawakilishi waandamanaji hao kujiondoa katika mazungumzo na wajume wa serikali. Wanafunzi hao wa vyuo vikuu vya Hon Kong walikua wamekubali kushiriki mazungumzo na serikali yaliyokua yameandaliwa na Waziri mkuu wa China, Leung Chun-ying. Hata hivo kumetokea machafuko leo Ijumaa jioni kufuatia makabiliano kati ya watetezi wa demokrasia na wapinzani wao.

Katika mtaa wa kibiashara wa Mongkok, waandamanaji wamekua wakipiga kelele, wakiomba warejeshewe mtaa wao wa Mongkong. “ Sisi wakaazi wa Hong Kong tunahitaji kupata chakula, nendeni vijijini kwenu”, wamekua wakisema waandamanaji hao, huku mamia ya watu wengine wakianza kushambulia waandamanaji hao na kufaanikiwa kuonda vizuizi viliyokua vimewekwa barabarani. Polisi imelazimika kuingilia kati ili kuzima makabiliano hayo. Makabiliano kama hayo yameripotiwa pia katika mtaa mwengine wa kibiashara wa Causeway Bay.

Mapema asubuhi Ijumaa wiki hii, makabilano mapya kati ya waandamanaji na polisi yalijitokeza katika mitaa kunakopatikana ofisi za wizara mbalimbali. Baadhi ya waandamanji hao wanaotetea demokrasia wanatuhumu mahasimu wao kwamba wamekua wakisajili watu wenye ubavu ili kusababisha vurugu.

Makundi matatu muhimu ya waandamanaji yameapa kutoendelea kushiriki mazungumzo na serikali iwapo serikali haitowakataza watu ambao wanadaiwa na makundi hayo kwamba “ wamekuwa wakiandaa mashambulizi” dhidi ya waandamanaji.

Ijumaa asubuhi wiki hii, shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu limekua limekubali kushiriki mazungiumzo na katibu mkuu wa manispa ya jiji la Hon Kong, Carrie Lam, huku likionya kwamba licha ya mazungumzo hayo maandamano yataendelea hadi pale uchaguzi wa moja kwa moja utapewa nafasi. Wakati huo huo waandamanaji hao wamemtaka kwa mara nyingine tena Waziri mkuu, Leung Chun-ying kujiuzulu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.