Pata taarifa kuu
HONG KONG-MAANDAMANO

Serikali ya Uingereza yatowa wito wa utulivu katika kisiwa cha Hong Kong

Serikali ya Uingereza Mkoloni wa zamani wa Jimbo la Hong Kong, imetowa wito kwa waandamanji jijini humo kuwa na mazungumzo yenye kujenga wakati huu maandamano yakiendelea kuchacha yakudai serikali ya Pekin uhuru zaidi wa kisiasa.

Matangazo ya kibiashara

Kulinganan na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Uingereza amesema wanataraji kuona mazungumzo yenye kujenga na yenye lengo la kupiga hatuwa Kidemokrasia jijini Hong Kong na imetowa wito kwa pande zote kurejesha utulivu.

Wizara hiyo imekumbusha kwamba walikubaliana na seikali ya Pekin kuhusu mfumo wa uongozi wa eneo hilo kwa muda wa miaka hamsini (50) tangu makabidhiano kwa China mwaka 1997.

Serikali ya Uingereza imesema inaguswa na hali iliopo jijini Hong Kong, na kuomba pande zote hususan serikali ya Pekin kuwapa Uhuru wananchi kuandamana, lakini pia waandamanaji watekeleze haki yao hiyo ya msingi katika mazingira yanayo ruhusiwa na sheria.

Hali imeendelea kuwa tulivu jijini Hong Kong wakati huu maandamano yakiendelea
Hali imeendelea kuwa tulivu jijini Hong Kong wakati huu maandamano yakiendelea REUTERS/Tyrone Siu

Hayo yanajiri wakati huu waandamanaji wanaotaka mabadiliko ya kidemokrasia wakijiandaa kwa maandamano hii leo jumatatu usiku katika maeneo mbalimbali jimboni humo na kusababisha shughuli zote kudhorita katika jimbo hilo lililo chini ya umiliki wa serikali ya Pekin.

Kampeni ya kususia shughuli za serikali ilipiga kasi tangu majuuma kadhaa katika eneo hilo koloni la zamani la Uingereza na kuchukuwa sura mpya mwishoni mwa juma lililopita Hong Kong ikishuhudia ghasia kubwa ambazo hazijawahi kushuhudiwa tangu kukabidhiwa kwa China mwaka 1997.

Shughuli zimeparaganyika katika na kulinfaya jiji la Hong Kong kuwa katika hali isiokuwa ya kawaida. Polisi walilazimika kutumia nguvu za ziada katika kuwatanya waandamanaji, waliokusanyika katika kisiwa hicho cha Hong Kong.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.