Pata taarifa kuu
HONG KONG

Maelfu waandamana Hong Kong kushinikiza mabadiliko ya kisiasa

Maelfu ya waandamanaji huko Hong Kong wamekabiliana na polisi, muda mfupi tu baada ya kiongozi wa serikali katika eneo hilo kutangaza kuaanzisha mazungumzo kuhusu mabadiliko ya kisiasa na uchaguzi katika eneo hilo.

Waandamanaji Hong Kong siku ya Jumapili
Waandamanaji Hong Kong siku ya Jumapili REUTERS/Bobby Yip
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji wanasema wanataka uhuru zaidi wa kisiasa katika eneo hilo na uchaguzi wa huru na haki.

Kiongozi wa eneo hilo Leung Chun-ying hata hivyo hajasema ni lini mazungumzo hayo yataanza ili kuleta mabadiliko hayo yanayoshinikizwa na waandamanaji hao wengi wao vijana.

Waandamanaji Hong Kong
Waandamanaji Hong Kong REUTERS/Bobby Yip

Waandamanaji hao wamewashtumu polisi kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha kuwasambaratisha, kupita kiasi wakati wa maandamano hayo waliosema ni ya amani.

Mwandamanaji akisaidiwa baada ya kulemewa na mabomu ya kutoa machozi
Mwandamanaji akisaidiwa baada ya kulemewa na mabomu ya kutoa machozi REUTERS/Bobby Yip

Wanafunzi wamekuwa katika mstari wa mbele kuongoza maandamano hayo, ambayo wanasema yataendelea hadi pale mabadiliko hayo yatakapofanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.