Pata taarifa kuu
LIBYA-UJERUMANI-USALAMA-SIASA

Makubaliano ya kimataifa kuelekea amani ya kudumu Libya yafikiwa Berlin

Viongozi wa dunia wameapa kuhakikisha kuwa amani ya kudumu inarejea nchini Libya, baada ya kufungua mkutano wa amani kuhusu nchi hiyo jijini Berlin nchini Ujerumani hapo Jumapili Januari 19.

Kutoka kuhoto kwenda kulia Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Libya Ghassan Salamé, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas huko Berlin Januari 19.
Kutoka kuhoto kwenda kulia Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Libya Ghassan Salamé, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas huko Berlin Januari 19. © REUTERS/Axel Schmidt/Poo
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Uturuki, Ufaransa, Urusi na mwenyeji wao Kansela Angela Merkel ni miongoni mwa wakuu hao waliohudhuria mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na kiongozi wa wapiganaji wa upinzani Khalifa Haftar na kiongozi wa serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa Fayez al-Sarraj.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Maataifa Antonio Guteress ameyataka mataifa ya kigeni kuacha kuchochea vita nchini Libya kwa kutuma silaha na wanajeshi.

Viongozi wa nchi kuu zinazohusika katika mzozo nchini Libya wamekubaliana kuheshimu vikwazo vya silaha vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa dhidi ya Libya mwaka 2011 na Umoja wa Mataifa.

Katika mkutano uliofanyika katika mji mkuu wa Ujerumani, Berlin, viongozi hao kutoka nchi kumi na moja pia wamekubaliana kuachana na "kuingilia" kwa nchi ya kigeni katika mgogoro unaoendelea kuikumba Libya. Hata hivyo wengi wana mashaka kuhusu makubaliano hayo iwapo yatatekelezwa.

Wakati wa mkutano huo uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa, jijini Berlin, Nchi kumi na moja ikiwa ni pamoja na Urusi na Uturuki zimekubali kwamba hakuna "suluhisho la kijeshi" kwa mgogoro huo, ambao unendelea kuithiri Libya kwa karibu miaka 10, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema.

Washiriki katika mkutano huo pia wametoa wito kusitiha mapigano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.