Pata taarifa kuu
DRC-BEMBA-SIASA-USALAMA

Bemba arejea DRC kuimarisha upinzani Lamuka

Mwanasisa wa upinzani na makamu wa zamani wa rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Jean pierre Bemba yuko DRC tangu Jumapili Juni 23.

Mpinzani Jean-Pierre Bemba akiwasabahi wafuasi wake, kabla ya kufanya mkutano mkutano St Therese, Juni 23, 2019.
Mpinzani Jean-Pierre Bemba akiwasabahi wafuasi wake, kabla ya kufanya mkutano mkutano St Therese, Juni 23, 2019. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia wametumia mabomu ya machozi dhidi ya wafuasi wa kinara wa upinzani na makamu wa rais wa zamani wa DRC Jean-Pierre bemba aliyerejea hapo jana nchini mwake akitokea Brussels nchini Ubelgiji.

Ni ziara ya pili ya mwanasisia huyo nchini DRC baada ya kuachiliwa huru na mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC baada ya kutumikia kifungo cha miaka kumi gerezani.

Washirika wa Bemba wanasema kuwa kiongozi huyo amerejea kumuunga mkono aliyekuwa mgombea mkuu wa upinzani Martin Fayulu ambaye anashikilia kuwa ndiye mshindi halali wa uchaguzi wa mwezi Desemba mwaka jana.

Tayari vinara wengine wa upinzani kama vile Mbusa Nyamwisi na Moise Katumbi, wamerejea kutoka uhamishoni.

Wachambuzi wa siasa wanasema kuwa kurejea kwa Bemba huenda kukamtikisa rais Felix Tshisekedi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.