Pata taarifa kuu
SOMALI-SIASA-USALAMA

Rais wa Mali IBK amteua waziri mkuu mpya

Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita amemteua Waziri wa Fedha Boubou Cissee kuwa waziri mkuu mpya, siku chache tu baada ya aliyekuwa waziri mkuu hivi karibuni, Soumeylou Boubeye Maiga kujiuzulu na serikali yake.

Rais Ibrahim Boubacar Keïta (kwenye picha) amemteua Boubou Cissé kwenye nafasi ya Waziri Mkuu.
Rais Ibrahim Boubacar Keïta (kwenye picha) amemteua Boubou Cissé kwenye nafasi ya Waziri Mkuu. © Michele CATTANI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Uteuzi wa waziri wa fedha katika nchi ya Mali Boubou Cissee kuwa waziri mpya wa Mali, umekuja kumaliza hali ya mvutano wa kisiasa ulioanza kujitokeza hivi karibuni kati ya rais IBK na wanasiasa wa upinzani pamoja na wabunge ambao kujiuzulu kwa waziri Soumeylou Maiga kulifanyika siku moja kabla ya kikao cha kutokuwa na imani naye kufanyika, mwishoni mwa juma lililopita.

Ilitarajiwa kuwa wabunge wangepiga kura hiyo ya kutokuwa na imani na serikali ya waziri mkuu huyo akikabiliwa na ukosoaji mkubwa kwa kushindwa kukabiliana na kuzorota kwa hali ya usalama nchini humo.

Uteuzi wa waziri mkuu mpya Boubou Cissee ulitangazwa Jumatatu wiki hii na ofisi ya rais kupitia ukurasa wake wa twitter.

Cisse anatarajiwa kuunda baraza jipya la mawaziri baada ya kupata ruhusa ya serikali na vyama vya upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.