Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-JALAI-USALAMA

Ethiopia yatangaza maombolezo ya kitaifa ya siku moja

Siku moja baada ya ajali ya ndege ya shirika la ndege la Ethiopian Airlines kuua watu 157 kutoka mataifa 35, serikali ya Kenya imetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku moja.

Vipande vya ndege ya shirika la ndege la Ethiopia Airlines katika eneo la ajali karibu na mji wa Bishoptu, kusini magharibi mwa Addis Ababa, Machi 10, 2019.
Vipande vya ndege ya shirika la ndege la Ethiopia Airlines katika eneo la ajali karibu na mji wa Bishoptu, kusini magharibi mwa Addis Ababa, Machi 10, 2019. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Raia 32 wa Kenya ni miongoni wa abiria wote 157 waliopoteza maisha kufuatia hiyo ya ndege aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikisafiri kutoka Adis Ababa kuelekea Nairobi nchini Kenya.

Ajali hiyo ilitokea mapema Jumapili asubuhi baada ya ndege hiyo kuruka kutoka Uwanja wa ndege wa Bore Mjini Adis Ababa.

Taarifa ya awali ya kampuni ya ndege ya Ethiopian Airlines ilisema ndege hiyo ilibeba abiria kutoka mataifa 32 yakiwemo Marekani, Uingereza, China, India, Misri, Canada na Ufaransa

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed kupitia ukurasa wake wa Twitter alitoa salamu za rambirambi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.

Katika hatua nyingine, Waziri wa usafirishaji wa Kenya, James machari amesema serikali ya nchi hiyo imepeleka maofisa kadhaa eneo la ajali na kuwataka raia kuwa watulivu.

Katika hatua nyingine shirika la Marekani la Boeing lililotengeneza ndege hiyo limeeleza kusikitishwa kwake na ajali hiyo iliyoua abiria wote na kuongeza kuwa litatoa msaada wa kiufundi ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Ndege hiyo mpya aina ya Boeing 737 ambayo ilinunuliwa mwaka jana ilikua ikitokea jijini Addis Ababa kuelekea jijini Nairobi nchini Kenya kabla ya kuanguka muda mfupi baada ya kuruka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.