Pata taarifa kuu
DRCUNSC-SIASA-USALAMA

Mshindi wa uchaguzi DRC kutangazwa kwa muda wowote kuanzia sasa

Matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Desemba 30 yanatarajiwa kutangazwa kwa muda wowote kuanzia sasa, kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi chini humo (CENI).

Ulinzi mkali umeimarishwa kwenye makao makuu ya Tume ya Uchaguzi CENI, KInshasa.
Ulinzi mkali umeimarishwa kwenye makao makuu ya Tume ya Uchaguzi CENI, KInshasa. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Matokeo ya uchaguzi ambayo yalitarajiwa kutangazwa siku ya Jumapili Januari 6 yaliahirishwa kwa madai kuwa Tume ya Uchaguzi (CENI) ilikuwa tayari imehesabu tu asilimia 20 ya kura zilizopigwa nchini kote.

Tume ya Uchaguzi inasema kuwa kwa muda wowote leo Jumatano au kesho Alhamisi mshindi wa uchaguzi wa urais anaweza kutangazwa.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini DRC, CENI Corneille Nangaa, amesema wanalo jukumu kubwa la kumaliza kazi iliyoko mbele yao na kwamba wanajitahidi kutangaza matokeo hayo katikan kipindi cha saa 24 au 48 zijazo.

Hata hivyo, chanzo kutoka CENI kinabaini kwamba hadi Jumanne jioni asilimia 80 ya kura ndizo zimekuwa zimekwisha hesabiwa.

Wakati huo huo mmoja kati ya viongozi wakuu wa upinzani, Martin Fayulu amesema kuwa wananchi wa DRC "wanamfahamu msindi" na kuionya Tume ya Uchaguzi "dhidi ya jaribio lolote la kuficha ukweli wa matokeo ya uchaguzi".

Mvutano wa kisiasa unaendelea nchini DRC wakati huu wananchi wa taifa hilo kubwa Afrika ya Kati wakiendelea kusubiri matokeo ya uchaguzi.

Polisi wamefunga njia barabara kuu ya Boulevard inayoelekea katika makao makuu ya ofisi za CENI wakati huu upinzani ukionya kuhusu kutangazwa kwa matokeo tofauti na yale wanayofahamu wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.