Pata taarifa kuu
DRC-KATUMBI-SIASA-USALAMA

Wafuasi wa Moise Katumbi waandamana DRC

Wafuasi wa mwanasiasa wa upinzani Moise Katumbi wameingia mitaani Jumatatu wiki hii katika mji wa Lubumbashi wakiomba kiongozi wao kurejea nchini DRC.

Wafuasi wa mwanasiasa wa upinzani DRC Moise Katumbi Chapwe wakiandamana mbele ya Mahakama Kuu Juni 27, 2018.
Wafuasi wa mwanasiasa wa upinzani DRC Moise Katumbi Chapwe wakiandamana mbele ya Mahakama Kuu Juni 27, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati ambapo rais Joseph Kabila anaendelea kusalia kimya wakati ambapo zimesalia siku mbili tu kabla ya kumalizika muda wa mwisho wa kuwasilisha fomu za kuwania uchaguzi mkuu ambao umepangwa kufanyika Desemba 23.

Muungano wa vyama vinavyoongozwa na Katumbi, Ensemble, vimeandaa maandamano katika maeneo mbalimbali ya nchi, lakini maandamano hayo yametawanywa na vikosi vya usalama, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

Polisi wamepiga risasi hewani na kuwakamata waandamanaji, ambao baadhi yao waliachiliwa haraka. Mwanasheria wa Katumbi, Peter Mbala, pia ameliambia shirika la habari la AFP kwamba aliona vijana wakimatwa katikati mwa mji, "karibu vijana ishirini" amesema.

"Tunataka Katumbi kurudi nchini Congo bila kuchelewa," waliandika waandamanaji hao kwenye mabango yaliyokua yakishikiliwa na wanawake ambao walikua miongoni mwa waandamanaji, kulingana na video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii.

Rais Kabila, ambaye Katiba haimruhusu kuwania muhula wa tatu ameendelea kusalia kimya ikiwa zimesalia ziku mbili kabla ya kufikia tarehe ya mwisho (Jumatano) ya wagombea urais kuwasilisha fomu za kuwania katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Desemba 23.

"Hadi wakati huu, hakuna sababu kwamba tunaweza kuahirisha tarehe ya mwisho kwa zoezi hili," Corneille Nangaa, Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ameliambia shirika la habari la AFP.

Siku ya Alhamisi na Ijumaa wiki jana rais Kabilaalizuru nchi jirani ya Angola, ambayo inafuatilia kwa karibu mchakato wa uchaguzi nchini DRC.

Hapo awali, aliwatuma Waziri wake wa Mambo ya Nje, mkuu wa Idara ya Upelelezi (ANR) na mkuu wa idara ya ujasusi katika nchi jirani ya Rwanda kukutana na rais Paul Kagame.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.