Pata taarifa kuu
SOMALIA-UN-SIASA

Umoja wa Mataifa wasema wanajeshi wa AMISOM hawawezi kupunguzwa kwa sasa Somalia

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limechelewesha zoezi la kuwaondoa wanajeshi wa kulinda amani nchini Somalia.

Jeshi la AMISOM kutoka Ethiopia likipiga doria nchini Somalia
Jeshi la AMISOM kutoka Ethiopia likipiga doria nchini Somalia TOBIN JONES / AU UN IST / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress amesema, hatua hii imekuja baada ya kubainika kuwa, wanajeshi wa Somalia bado hawajapata mafunzo ya kutosha kuachiwa usalama wa nchi hiyo.

Umoja wa Mataifa una wanajeshi 1,000 ambao wanashirikiana na wanajeshi wa Umoja wa Afrika AMISOM wapatao 20,000 ambao wanapambana na wanamgambo wa Al Shabab.

Guteress ameliandikia barua Baraza la Usalama na kuliambia kuwa, haitawezekena tena kuwapunguza wanajeshi wa AMISOM kufkia mwezi Oktoba kama ilivyopangwa.

Hatua hii imesababisha Baraza hilo kuamua kuwa wanajeshi hao wa AMISOM sasa waondoke nchini humo kufikia tarehe 31 mwezi Mei mwaka 2019.

Mamia ya watu wamepoteza maisha mwaka huu pekee katika mashambulizi ya kundi la Al Shabab.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.