Ufaransa kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na Misri
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean yves Ledrian amesema ufaransa iko tayari kuhakikisha ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi yake na Misri unaimarika zaidi katika mapambano dhidi ya ugaidi.
Imechapishwa:
Ledrian aliyasema hayo punde baada ya kukutana na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi jijini Cairo wakati wa ziara yake siku ya Jumapili, lakini pia kuzungumzia masuala ya biashara na hali ya Libya.
Mataifa haya mawili, yanaridhishwa na hali ya utulivu ambao umeanza kushuhudiwa nchini Libya kuelekea Uchaguzi Mkuu baadaye mwaka huu.
Ufaransa imeendelea kuunga mkono serikali ya Umoja nchini Libya na kupatikana kwa suluhu kuhusu mgogoro huo unaoendelea nchini humo.
Machafuko nchini Libya yaliyozuka baada ya kifo cha rais wa nchi hiyo Moamar Kaddafi, yamesababisha vifyo vya watu wengi na wengine wengi kulazimika kuyahama makazi yao.