Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Buhari aitishwa mbele ya bunge kuhusu vurugu nchini Nigeria

Bunge la Nigeria limemuitisha Rais Muhammadu Buhari kuelezea hatua zilizochukuliwa kupunguza vurugu zinazoendelea kuongezeka katika majimbo ya katikati mwa nchi hiyo.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari. REUTERS /Stringer
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano wiki hii wabunge walipiga kura hoja ya kumtaka Rais Buhari kujieleza mbele ya bunge na kutaka wakuu na washauri katika vikosi vya usalama na ulinzi kuondolewa kwenye nafasi zao, kwa mujibu wa Spika wa bunge, Yakubu Dogara.

Rais Buhari, ambaye pia ni amiri jeshi mkuu, "anatarajia kujibu maswali nyeti kuhusu kile ambacho serikali inafanya ili kukomesha mfululizo wa mauaji katika majimbo mbalimbali ya nchi ya Nigeria ", Spika wa bunge ameongeza kwenye ukurasa wake wa Twitter.

"Wajibu mkuu wa serikali ni kuhakikisha usalama wa watu na mali na, kama bunge tliopewa mamlaka haya na raia, hatuwezi kuendelea kuangalia watu wetu wakiuawa kiholela" amesema Yakuba Dogara.

Vurugu nyingi zimekua zikitokea katika jimbo la Benue ambako watu 385 wameuawa tangu mwezi Januari, kwa mujibu wa shirika la Marekani la Armed Conflict Location ande Event Data Project, linalojihusisha katika migogoro ya kivita.

Siku ya Jumanne wiki hii, mapadri wawili na waumini 16 waliuawa kwa kupigwa risasi na kundi la wahalifu zaidi ya thelathini, katika sherehe ya mazishi katika kijiji cha jimbo la Benue, kwa mujibu wa polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.