Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-CHINA-USHIRIKIANO

Emmerson Mnangagwa azuru China

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa anazuru China, mshirika wa kihistoria wa nchi hiyo, kwa ziara ya serikali ya siku tano. Ziara hii ya siku nyingi kama hizi inathibitisha uhusiano wa zamani wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akitembelea Kituo cha nguvu ya umeme cha Kariba Machi 28, 2018.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akitembelea Kituo cha nguvu ya umeme cha Kariba Machi 28, 2018. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

China ni mwekezaji mkubwa wa kigeni nchini Zimbabwe. Lakini Emmerson Mnangagwa na Xi Jinping wanatarajiwa pia kuzungumzia siasa kwa sababu ya ushiriki wa China katika masuala ya Zimbabwe.

Uhusiano kati ya China na Zimbabwe ni wa muda mrefu, tangu vita vya Rhodesia. Wakati huo waasi wa Joshua Nkomo walisaidiwa na Moscow, huku wale wa Robert Mugabe wakisaidiwa na China. Vita vya wakati huo, ambapo rais wa sasa wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, alikua kwenye mstari wa mbele, pia vilianzishwa kijeshi nchini China.

China ilimsaidia Robert Mugabe alipokua akiongoza kundi moja la waasi nchini nchini Zimbabwe, na pia ilimsaidia na kuwa mshirika wake alikpokua rais tangu mwaka 1980. Wakati Umoja wa Ulaya uliweka vikwazo dhidi ya Zimbabwe mwaka 2003, mahusiano na China yaliimarishwa mara zaidi. China ni msaidizi wa kimataifa wa Mugabe. Robert Mugabe alizuru China mara kumi na tano. Ziara yake ya mwisho ilikua mwaka 2017.

Kwa mshangao mkubwa, China haikuonyesha msimamo wake kufuatia kung'atuliwa madarakani kwa Robert Mugabe mwezi Novemba, ikisema ataendelea kuwa "rafiki mzuri" wa Jamhuri ya Watu wa China.

Siku moja baada ya jeshi kupindua serikali, mkuu wa majeshi ya Zimbabwe Chiwenga alifanya ziara ya siri nchini China. Wakati huo wengi walijiuliza kama kweli ilikua ni ziara ya kikazi au njia ya kupata idhni kutoka kwa serikali ya China ya kumtimua Robert Mugabe.

China, mwekezaji anayeongoza

China, mshirika wa kisiasa, lakini pia mshirika mwaminifu wa kiuchumi. Wachina wamekuwa wakiwekeza kwa wingi katika uchumi wa Zimbabwe kwa miaka yote hiyo. Biashara imekua ikiongezeka kwa karibu euro bilioni moja kati ya nchi hizi mbili kila mwaka.

Makampuni ya China yana ushirikiano wa karibu na jeshi la Zimbabwe, yapo katika sekta ya ujenzi, barabara, biashara, pamba, madini na hasa tumbaku, ambapo China ni mnunuzi mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.