Pata taarifa kuu
MALI-UN-USALAMA

Askari wanne wa Umoja wa Mataifa wauawa Mali

Wanajeshi wanne wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa wameuawa na wengine wanne kujeruhiwa vibaya katika mlipuko wa mgodi katikati mwa nchi ya Mali.

Askari wa kulinda amani nchini Mali (Minusma), hapa ni katika mji wa Kidal, 22 Julai mwaka 2015.
Askari wa kulinda amani nchini Mali (Minusma), hapa ni katika mji wa Kidal, 22 Julai mwaka 2015. REUTERS/Adama Diarra
Matangazo ya kibiashara

Vyanzo vya kiusalama vimesema mlipuko huo ulitokea majira ya alasiri wakati gari lililokuwa limewabeba askari zaidi ya kumi wa umoja wa mataifa lilipokanyaga kitu kinachosadikiwa kuwa kilipuzi kati ya maeneo ya Boni na Douentza katika kanda ya Mopti, katikati mwa nchi hiyo.

Afisa wa jeshi la serikali ya Mali ameviambia vyombo vya habari kwamba janga hili jipya limefanya idadi ya askari wa kikosi hicho cha kulinda amani ambao wamepoteza maisha nchini Mali tangu mwanzo wa mwaka huu kufikia nane.

Umoja wa mataifa umesema wanajeshi wake wamekuwa wakikabiliwa na hali ngumu ya kudhibiti mashambulizi ya aina hii, kwa kuwa hadi sasa imekuwa kama kitenda wili kumtambua adui anayetekeleza aina hii ya mashambulizi kwa kutumia vilipuzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.