Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-USALAMA-HAKI

Mchungaji Evan Mawarire akamatwa Zimbabwe

Polisi nchini Zimbabwe wamemkamata Mhubiri maarufu Evan Mawarire ambaye pia ni mwanaharakati wa kisiasa baada ya mahubiri siku ya Jumapili.

Mchunganji Evan Mawarire uchochezi kupitia mitandao ya kijamii
Mchunganji Evan Mawarire uchochezi kupitia mitandao ya kijamii MUJAHID SAFODIEN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Polisi wanamshutumu kwa kuandika ujumbe wa uchichezi kupitia mitandao ya kijamii na kueleza kuwa serikali ya rais Robert Mugabe imeshindwa kuimarisha uchumi.

Mchungaji huyo amekuwa katika harakati za kumkosoa rais Mugabe na kuongoza maandamano kadhaa tangu mwaka 2016.

Mwezi Juni Mhubiri Evan Mawarire alifikishwa Mahakamani kujibu mashtaka ya uchochezi.

Wakati huo Bw Mawarire alifunguliwa mashtaka ya kushiriki katika mkutano usio halali na kusababisha usumbufu, madai ambayo aliyakanusha.

Mwezi Julai, alikamatwa kwa uchochezi na kuandaa maandamano dhidi ya rais Robert Mugabe na kesi yake inatarajiwa kusikilizwa mwezi Septemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.