Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Boko haram yawaachia huru Wasichana 82 wa Chibok nchini Nigeria

Serikali ya Nigeria imesema wasichana 82 wa shule  wameachiwa huru baada ya kutekwa na wapiganaji wa kiislamu Boko haram takribani miaka mitatu iliyopita katika eneo la Chibok.

Wasichana wa shule waliotekwa na wapiganaji wa kiislamu Boko haram nchini Nigeria
Wasichana wa shule waliotekwa na wapiganaji wa kiislamu Boko haram nchini Nigeria rfi
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa serikali ya nigeria majadiliano kuhusu kuachiwa kwa zaidi ya wasichana mia mbili wa shule waliotekwa na kundi la wapiganaji wa boko haram kwa zaidi ya miaka mitatu yalifanyika na na kufanikisha kuachiwa kwao kwa makubaliano ya kubadilishana wafungwa ambao ni waiganaji wa kundi hilo waliokuwa wakishikiliwa na serikali.

Ikulu ya Nigeria imetangaza kuwa miezi ya mazungumzo kati yake na wapiganaji hao wa kiislamu imezaa matunda,kwa takribani miezi sita tangu wanafunzi 21 kuachiwa kwa msaada wa wasuluhishi wa kimataifa.

Serikali imedai kuwa atimaye idara za usalama nchini humo zimewarejesha wasichana hao kwa kubadilishana watuhumiwa wa kundi hilo waliokuwa wakishikiliwa na mamlaka.
Hata hivyo hakuna ufafanuzi zaidi uliotolewa kuhusu idadi ya watuhumiwa walioachiwa wala utambulisho wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.