Pata taarifa kuu
UFARANSA

Kesi dhidi ya mtoto wa rais Obiang Nguema ya ahirishwa Ufaransa

Mahakama moja nchini Ufaransa imekubali kuahirisha kesi ya rushwa dhidi ya mtoto wa rais wa Equatorial Guinea ambaye pia ni makamu wa rais wa nchi hiyo, baada ya kukubaliana na ombi la upande wa utetezi.

Teodorin Nguema Obiang, hapa akiwa mjini Malabo mwaka 2013
Teodorin Nguema Obiang, hapa akiwa mjini Malabo mwaka 2013 AFP
Matangazo ya kibiashara

Tarehe mpya za kuanza kwa kesi hiyo iliyoanza Jumatatu ya tarehe 2 Januari, inajadiliwa huku jaji kiongozi kwenye kesi hiyo akipendekeza kuwa tarehe 19 ya mwezi huu.

Teodorin Obiang, anatuhumiwa kwa kutumia zaidi ya euro milioni 100 fedha za uma, kununulia vitu vya thamani ikiwemo magari na nyumba kwenye mji mashuhuru kwa kuwa na matajiri wengi wa jiji la Paris.

Kesi hii ambayo ni ya kwanza kufanywa na Ufaransa baada ya kufanya uchunguzi wao kwa viongozi wa Afrika wanaotuhumiwa kwa rushwa za ubadhirifu wa mali za uma huku wananchi wao wakiendelea kutaabika.

Timu ya mawakili wa Obiang wameiambia mahakama kuwa, muda wa wiki moja ijayo uliokuwa umepangwa na mahakama hiyo kuanza kusikiliza kesi hiyo, hautatosha na kuwapa wao nafasi ya kuwaita mashahidi.

Obiang, mwenye umri wa miaka 47 na mtoto wa rais Teodoro Obiang Nguema, alijaribu kuzuia kesi hiyo kwenda mahakani akidai mwanae hana hatia, akisema fedha hizo zimetoka kwenye njia salama na sio rushwa au fedha za uma kama inavyodaiwa na waendesha mashtaka wa Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.