Pata taarifa kuu

Said Djinnit atoa wito wa kuendeleza mchakato wa kisiasa

Mjumbe Maalum wakatibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na ukanda wa maziwa makuu, Said Djinnit, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa muda umewadia wa kuitaka serikali ya DRC kufanya linalowezekana ili kuandaa mazungumzo ya kisiasa yatakayowashirikisha wanasiasa kutoka pande zote.

Saïd Djinnit, Mjumbe Maalum wake katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na ukanda wa maziwa makuu.
Saïd Djinnit, Mjumbe Maalum wake katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na ukanda wa maziwa makuu. AFP/SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

Mjumbe Maalum wakatibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na ukanda wa maziwa makuu amezitaka pande zote kutekeleza malengo yao ya kisiasa kwa njia ya amani na mazungumzo.

Wakati huo huo serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo imepiga marufuku maandamano yoyote nchini humo, na kuwataka wanasiasa kuiheshimu sheria, hatua ambayo wanaharakati wanasema ni kinyume na haki za wananchi.

Serikali ya jimbo la mji mkuu wa Kinshasa kupitia msemaji wake Therese Kalonda imejitetea kulingana na katiba.

Hayo yanajiri wakati wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambao wataongozwa na Angola pamoja na Ufaransa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wiki ijayo kutathmini hali ilivyo katika nchi hiyo, wakati huu wapinzani wenye msimamo mkali wakipinga kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais hadi Aprili mwaka 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.