Pata taarifa kuu
NTAGANDA-ICC

Boscos Ntaganda aendelea kugoma kula, ashinikiza kusikilizwa

Kiongozi wa zamani wa waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, Bosco Ntaganda, Jumatatu ya wiki hii ameingia katika siku yake ya 12 ya mgomo wa kula kwenye gereza anakoshikiliwa nchini Uholanzi, huku akikataa kuhudhiria vikao vya kesi yake.

Bosco Ntaganda, kiongozi wa zamani wa kundi la waasi nchini DRC.
Bosco Ntaganda, kiongozi wa zamani wa kundi la waasi nchini DRC. REUTERS/Michael Kooren
Matangazo ya kibiashara

Wakati mmoja akiwa kiongozi wa waasi aliyeogopewa zaidi nchini DRC, jatokea mbele ya majaji wa mahakama hiyo iliyoko mjini The Hague, toka tarehe 7 ya mwezi September mwaka huu.

Ntaganda anakuwa mfungwa na mtuhumiwa wa kwanza katika mahakama hiyo, kufanya mgomo wa kula toka mahakama hiyo ilipoundwa mwaka 2002, kusikiliza kesi za wahalifu wa kivita kidunia.

Licha ya mgomo wake majaji wanaosikiliza kesi yake wameagiza kesi hiyo kuendelea hata kama Ntaganda hatatokea mahakamani.

Mawakili wake ambao alikataa wasimtete mbele ya mahakama hiyo, wamesema kuwa hawajui ni lini mteja wao ataacha mgomo wa kula, na kwamba suala hilo wanawaachia majaji wa mahakama hiyo.

Ntaganda ambaye amekuwa akizuiliwa kwenye jela moja ya mahakama hiyo iliyoko nje kidogo ya jiji la The hague toka alipojisalimisha mwaka 2013, amewataka mawakili hao kuacha kumuwakilisha.

Akifahamika kama Terminator wakati mmoja, Ntaganda amekanusha mashtaka 18 ya uhalifu wa kivita yanayomkabili mbele ya mahakama ya ICC.

Jaji kiongozi kwenye kesi hiyo, amesema kuwa amepokea ripoti ya kiongozi wa jela ambako Ntaganda anashikiliwa, na kwamba anaonesha kuwa mchovu lakini hali yake sio ya kuhatarisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.