Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Burkina Faso: makubaliano ya kutuliza ghasia yasainiwa kati ya majeshi

media Katika Kasri la Mogho Naba, Mfalme wa jamii ya Mossi (katikati akivaa nguo za kiraia), wanajeshi wa vikosi vya jeshi vinavyounga mkono serikali ya mopito na afisa wa kikosi cha ulinzi wa Rais (RSP) wakisaini makubaliano ya kutohasimiana Jumanne Septemba 22 RFI/Olivier Rogez

Nchini Burkina Faso, vikosi vya jeshi vinavyounga mkono serikali ya mpito na afisa wa wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa Rais (RSP) wamesaini mkataba wa kutoshambuliana usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano.

Wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa Raisa (RSP) wamekubali kurudi kambini na vikosi vya jeshi vinavyounga mkono serikali ya mpito kurudi nyuma kilomita 50 karibu na mji mkuu.

Hata hivyo wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa Rais hawakuweka chini silaha kama ilivyokua imeombwa na vikosi vya jeshi vinavyounga mkono serikali ya mpito. Mapema Jumanne jioni, jenerali Diendéré alihakikisha kuwa Michel Kafando ataachiliwa huru rasmi leo Jumatano.

Makubaliano hayo yamesainiwa Usiku wa Jumanne mjini Ouagadougou kati ya vikosi vya jeshi vinavyounga mkono serikali ya mpito na wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa Raiswaliofanya mapinduzi. Ni makubaliano ya kuepusha machafuko ambayo yanaeleza kwamba kikosi cha ulinzi wa Rais (RSP) kinachoongozwa na jenerali Diendéré kitasalia kambini katika kambi yake wakati ambapo vikosi vya jeshi vinavyounga mkono serikali ya mpito vitarudi nyuma kilomita hamsini na mji mkuu.

Makubaliano hayo yamesaini rasmi mbele ya Mogho Naba, Mfalme wa jamii ya Mossi na kiongozi wa kiroho nchini Burkina Faso. Makubaliano hayo yalitiliwa saini na Korogho Abdulaziz, Kaimu mkuu wa kikosi cha ulinzi wa Rais (RSP), na maafisa wanne waliotumwa na vikosi vya jeshi vinavyounga mkono serikali ya mpito. Baadhi ya viongozi wa wakuu wa vikosi vya jeshi vinavyouunga mkono serikali ya mpito ambao walianzisha jitihada ya kuelekea katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou ni wanafahamiana na wale wa kikosi cha ulinzi wa Rais (RSP).

Wakati huo huo ujumbe wa ECOWAS unaoundwa na marais kutoka jumuiya hiyo, unatarajia kuwasili mjini Ouagadougou ili kuendelea na mashauriano kati ya pande hizo mbili na kujadili kuhusu kumrejesha mamlakani Rais Michel Kafando na taasisi zingine za mpito.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana