Pata taarifa kuu
MAURITIUS-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi na marekebisho ya Katiba Mauritius

Takribani wapiga kura 937,000 wamejieleleza katika vituo vya kupigia kura 317 vilivyovunguliwa mapema asubuhi Jumatano Desemba 10 nchini Mauritius.

Waziri mkuu anaye maliza muda wake Mauritius, Navim Ramgoolam (kushoto) na Waziri mkuu wa zamani Sir Anerood Jugnauth (katikati), wagombea kwenye wadhifa wa Waziri mkuu Mauritius.
Waziri mkuu anaye maliza muda wake Mauritius, Navim Ramgoolam (kushoto) na Waziri mkuu wa zamani Sir Anerood Jugnauth (katikati), wagombea kwenye wadhifa wa Waziri mkuu Mauritius. AFP/ ALI SOOBYE
Matangazo ya kibiashara

Raia wa nchi hiyo watamchagua kiongozi wao kati ya wagombea wawili ambao ni Navin Ramgoolam, Waziri mkuu anaye maliza muda wake, na Waziri mkuu wa zamani Sir Anerood Jugnauth.

Navin Ramgoolam anataka kufanyike marekebisho ya Katiba ili aanzishe mfumo mpya wa uongozi wa nchi ambapo rais atachaguliwa kwa kipindi cha miaka saba. Jambo ambalo linapingwa na rais wa zamani Sir Anerood Jugnauth.

Alipokua katika kampeni ya uchaguzi, Navin Ramgoolam alisema kuna uwezekano wa kuanzishwa kwa jamhuri mpya na marekebisho ya katiba.
Lengo lake: ni kuwa rais mwenye hadhi na nguvu mpya kwa muda wa miaka saba madarakani.

Ili kutimiza ndoto yake ya zamani, Waziri mkuu anayemaliza muda wake na kiongozi wa Labour Party amekihusisha katika mradi wake chama kingine chenye ushawishi mkubwa nchini humo, cha Paulo Berenger. Vyama Vyote hivyo viwili vinawakilisha 80% ya wapiga kura. Vyama vyote hivyo vinavyojumuika katika muungano huo, vina imani kwamba vitashinda kwa jumla ya viti vyote 60 na kuweza kupitisha muswada wamarekebisho ya Katiba kufutia wingi wa viti Bungeni.

Lakini muungano unaoongozwa na Sir Anerood Jugnauth, unaweza kuharibu mipango yao, kwa mujibu wa waangalizi wengi. Pamoja na umri wake wa miaka 84, waziri mkuu wa zamani alifanya kampeni iliyowashangaza wengi. alibaini kwamba hatokubaliana na jaribio la kufanya marekebisho ya Katiba, lakini alitangaza mfululizo wa miradi yake ambayo imeoneka kuvutia sehemu kubwa ya wapiga kura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.