Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-PISTORIUS-Sheria

Kesi ya Pistorius yarejeshwa mahakamani

Aliye kuwa mwanariadha mlemavu kutoka Afrika Kusini, Ocar pistorius anatarajiwa kufikishwa tena mahakamani.

Mwanariadha wazamani wa Afrika Kusini Oscar Pistorius.
Mwanariadha wazamani wa Afrika Kusini Oscar Pistorius. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Jumatano Desemba 10 asubuhi, jaji ameruhusu kesi hiyo isikilizwe katika kitengo cha rufaa, baada ya viongozi wa Mashitaka kukataa rufaa kwa hukumu aliyopewa Oscar Pistorius.

Baada ya miezi minane kesi yake ikisikilizwa, Oscar Pistorius alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kumuua bila kukusudia mpenzi wake Reeva Steenkamp mwezi Februari mwaka 2013. Hukumu ambayo Ofisi ya Mashitaka haikukubaliana nayo.

Kwa sasa kesi imefikishwa mbele ya Korti kuu ya rufaa, ambayo itatathmini kwa kina hukumu aliyopewa Oscar Pistorius iwapo inaendana na kosa alilofanya.

Majaji walimkuta Oscar Pistorius na kosa la kuua bila kukusudia, lakini Ofisi ya Mashitaka haikukubalina na uamzi wa majaji.

Kulingana na sheria ya Afrika Kusini, Oscar Pistorius hatasikilizwa, lakini majaji watatathmini kosa pamoja na hukumu aliyopewa.

Jaji Thokozile Masipa alibaini kwamba Ofisi ya Mashitaka haikuonyesha ushahidi tosha kuwa pistorius alikua na nia ya kuua. Lakini Mwendesha mashitaka aliona kuwa risasi nne alizoyofyatuliwa Reeva Steenkamp ni ushahidi tosha kuwa Pistorius alikua na nia ya kuua. Pistorius anakabiliwana kifungo cha miaka 15.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.