Pata taarifa kuu
ARFIKA KUSINI-Pistorius-Sheria

Afrika Kusini: Oscar Pistorius ahukumiwa kifungo cha miaka 5 jela

Mwanariadha wa zamani wa Afrika Kusini anaeishi na ulemavu, Oscar Pistorius amehukumiwa leo Jumanne kifungo cha miaka mitano jela, baada ya kesi yake kuendeshwa kwa muda wa miezi saba, na kusikilizwa kwa muda wa siku 48.

Mwanariadha wazamani wa Afrika Kusini Oscar Pistorius akiwa Mahakamani.
Mwanariadha wazamani wa Afrika Kusini Oscar Pistorius akiwa Mahakamani. Reuters / Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ilifuta tuhuma za kuua kwa makusudi ziliyokua zikimkabili Pistorius kwa kukosa vithibitisho kutoka upanda wa mashtaka, lakini Mahakama ilimkuta na hatia ya kuua bila kukusudia.

Awali upande wa mashtaka ulimuombea Pistorius adhabu ya kifungo cha miaka 10 jela, lakini upande wa utetezi ulisema haukubaliane na adhabu hio kutokana na ukosefu wa ushahidi wa kutosha na badala yake uliomba Pistorius apewe kifungo cha nyumbani.

Mwakilishi wa Idara ya Magereza ya Afrika Kusini Joel Maringa alipendekeza kuwa Oscar Pistorius aadhibiwe kwa kupewa kifungo cha nyumbani kwa kipindi cha miaka mitatu pamoja na huduma za jamii kwa kupatikana na hatia ya kumuua mchumbake Reeva Steenkamp. Pistorius alipatikana na hatia mwezi uliopita kwa kumpiga risasi na kumuua mchumba wake bila kukusudia mnamo mwaka wa 2013.

Mwendesha mashtaka wa serikali Gerrie Nel alilitaja pendekezo la Maringa kuwa “lisilofaa”. Wakati akimhoji shahidi huyo, Nel alimuuliza Maringa kama alifahamu uzito wa uhalifu ambao Pistorius aliufanya, baada ya kukiri kuwa hakuwa na ufahamu wa kina kuhusu kesi hiyo.

Maringa alikuwa mmoja wa mashahidi watatu walioitwa na mawakili wa Pistorius ambao wanataka mshtakiwa apewe kifungo cha nyumbani.

Katika utetezi wake majuma kadha yaliyopita, mwanasheria wa Pistorius alibaini kwamba mteja wake alipoteza mambo mengi kiwa ni pamoja na mpenzi wake Reeva Steenkamp , akisema kwamba kumuweka jela atakabiliwa na matatizo mengi zaidi.

Uamuzi aliofanya jaji Thokozile Masipa uliwashangaza na kuwakasirisha Waafrika Kusini wengi wakiwemo mawakili ambao waliamini kuwa alitumia vibaya tafsiri ya mauaji, na wakahoji kama mfumo wa mahakama unashindwa kufanya kazi vyema katika nchi hiyo yenye kiwango kikubwa cha uhalifu.

Kabla ya uamzi huo kutolewa, Mwendesha mashtaka alisema, iwapo Pistorius hatapewa adhabu ya kifungo jela, raia wa Afrika Kusini wataona kuwa wamefanyiwa unyonge.

Kwa  muda wote ambapo kesi yake ilikua ikisikilizwa, Pistorius alikua nje kwa dhamana ya dola milioni 90,000. Alilazimika kuuza nyumba yake ya kifahari mjini Pretoria ili kufadhili gharama ya kesi hiyo na pia alijiondoa kutoka mashindano ya riadha tangu alipokamatwa. Hukumu dhidi yake inasubiriwa kutolewa leo Jumanne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.