Pata taarifa kuu
RWANDA-Mauaji ya kimbari

Ufaransa yasusia maadhimisho ya miaka 20 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda

Ufaransa imejiondoa kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya mauaji ya kimbari ya nchini Rwanda baada ya Rais Paul Kagame kwa mara nyingine tena kuishutumu Paris kushiriki katika mauaji hayo makubwa mwaka 1994 . 

Rais wa Rwanda Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul Kagame nairobiwire.com
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje Romain Nadal amesema Ufaransa imeshangazwa na shutuma za rais Kagame, ambazo zinakwenda kinyume na juhudi za maridhiano kati ya nchi hizo mbili na kutangaza kuwa Waziri wa Sheria Christiane Taubira hatohudhuria maadhimisho hayo yatakayofanyika kesho Jumatatu mjini Kigali.

Akizungumza na gazeti la kila wiki la Jeune Afrique jana Jumamosi ,rais Kagame ameshutumu Jukumu la moja kwa moja la Ubelgiji na Ufaransa katika maandalizi ya kisiasa kwa ajili ya mauaji hayo ya kimbari mwaka 1994.

Takribani watu laki nane wakiwemo watutsi na wahutu waliokuwa wakipinga serikali ya rais Juvenile Habyarimana waliuawa katika machafuko hayo makubwa .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.