Pata taarifa kuu
DRC

Tume ya uchaguzi DRC yaahirisha kutangaza mshindi wa urais

Tume ya uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemoakrasia ya Kongo, CENI imeahirisha kutangaza kwa mshidi wa urais katika uchaguzi uliofanyaika wiki iliyopita.

Daniel Finnan
Matangazo ya kibiashara

CENI ilitarajiwa kumtagaza mshindi usiku wa kuamkia leo na inasema kuwa inahitaji muda zaidi wa kujumlisha matokeo yote kabla ya kutangaza mshindi.

Hata hivyo matokeo ya awali yanaonyesha kuwa Joseph Kabila anaongoza dhidi ya mpinzani wake Ettiene Tshishekedi.

Tume hiyo ya ucahguz sasa inasema itatangaza matokeo ya mwisho ndani ya saa 24 zijazo.

Msemaji wa tume hiyo Matthieu Mpita anasema kuahirishwa kutolewa kwa matokeo ya mwisho kumetokana na tume hiyo kutopata matokeo kutoka vituo 169 na hivyo kulingana na sheria haiwezi kutoa matokeo ya mwisho kabla ya matokeo yote kuwasilishwa.

Hali ya wasiwasi imeanza kujitokeza nchini humo hasa mjini Kinshasa, baada ya wakazi wa mji huo kuanza kuhamia maeneop mengine kutoka wasiwasi wa usalama wao.

Wasiwasi wa wananchi hao unakuja kutokana na hisia kuwa machafuko huenda yakatokea baada ya upinzani kupinga matokeo ya awali.

Hata hivyo usalama umeimarishwa ili kuhakikisha kuwa hakuna matukio yatakayosababisha machafuko ama uvunjifu wa amani.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.