Pata taarifa kuu
URUSI-UINGEREZA-DIPLOMASIA

Urusi yalipiza kisasi kwa kuwafukuza wanadiplomasia 23 wa Uingereza

Serikali ya Urusi imetangaza kuwafukuza wanadiplomasia 23 wa Uingereza, hali inayoendelea kuyumbisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Rais wa Urusi  Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin Anatoly Maltsev/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya nje ya Urusi imesema wanadiplomasia hao wa Uingereza wana wiki moja kuondoka nchini humo.

Hatua hii ya Urusi imeonekana kama kulipiza kisasi baada ya Uingereza kuwafukuza wanadiplomsia wake 23 wiki hii.

Hii ilikuja  baada ya uchunguzi kuonesha kuwa Moscow ilihusika katika jaribio la kumuua jasusi wake wa zamani Sergei Skripal na binti yake Yulia kwa kuwapa sumu hatari.

Pamoja na kuwafukuza wanadiplomasia hao, Urusi pia imefunga kituo cha kutoa mafunzo ya utamaduni wa Uingereza kufunga ubalozi wake mdogo  mjini Saint Petersburg.

Urusi imeendelea kukanusha kuwa ndio iliyohusika na tukio la kumpa sumu, jasusi huyo wa zamani ambaye anaendelea kupata matibabu nchini Uingereza.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amesema, hatua ya Urusi haitabadilisha msimamo wa nchi yake kuwa, Moscow ndio iliyompa sumu jasusi huyo wa zamani wa Urusi na Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.