Pata taarifa kuu
UTURUKI-EU

Uturuki yatishia kufungua mpaka wake kuruhusu wahamiaji kuingia Ulaya

Rais wa Uturuki, Racep Tayyip Erdogan ametishia kuufungua mpaka wa nchi yake, kuruhusu wahamiaji kuingia kwenye nchi za Ulaya, kauli ambayo huenda ikavunja makubalio yaliyopelekea kupungua kwa wahamiaji wanaoingia Ulaya. 

Baadhi ya wahamiaji wanaokimbia nchi zao kutaka kuingia barani Ulaya.
Baadhi ya wahamiaji wanaokimbia nchi zao kutaka kuingia barani Ulaya. REUTERS/Zohra Bensemra
Matangazo ya kibiashara

Matamshi ya Erdogan, ambayo ni makali kuwahi kuyatoa hivi karibuni dhidi ya umoja wa Ulaya, yamesababisha nchi ya Ujerumani kuonya kuhusu matamshi hayo, ikisema hayana msaada wowote kwa tatizo lililopo.

Tisho la Uturuki limekuja ikiwa ni siku moja tu baada ya bunge la Ulaya, kuikasirisha nchi ya Uturuki kwa kuunga mkono kusitishwa kwa mazungumzo ya kuipokea nchi hiyo kama mwanachama mpya wa umoja wa Ulaya.

Nchi za Ulaya zinasema zinasitisha mazungumzo na Uturuki, kutokana na kuguswa na namna ambavyo ukiukwaji wa haki za binadamu umeendelea kushuhudiwa nchini humo hasa baada ya kushinidikana kwa jaribio la mapinduzi.

Machi 18 mwaka huu, nchi ya Uturuki na Umoja wa Ulaya walifikia makubaliano kwa nchi ya Uturuki kuzuia wimbi la wahamiaji wanaopitia nchini mwake na kukubali kuwapokea sehemu ya wahamiaji waliofurushwa kwenye nchi za Ulaya, mpango ambao kwa sehemu kubwa umefanikiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.