Pata taarifa kuu
UGIRIKI-WAKIMBIZI

Wakimbizi wapigwa na butwaa baada ya kambi yao kuteketezwa kwa moto

Uvumi na hofu vimeendelea kutawala wakimbizi na wahamiaji katika kambi ya Moria, katika kisiwa cha Ugiriki cha Lesbos, baada ya kambi hiyo kuteketezwa kwa moto Jumatatu wiki hii. Kambi hii ilishambuliwa na moto mkubwa ambao inadaiwa kuwa uliwashwa kwa makusudi.

Kambi ya Moria, Ugiriki, iliteketezwa kwa moto na kupelekea wakimbizi kukimbilia katika maeneo jirani.
Kambi ya Moria, Ugiriki, iliteketezwa kwa moto na kupelekea wakimbizi kukimbilia katika maeneo jirani. REUTERS/Giorgos Moutafis
Matangazo ya kibiashara

Hali hiyo ilisababisha karibu watu 4,000 waliokua wakipewa hifadhi katika kambi hiyo kukimbilia katika maeneo jirani ili kuepuka moto huo.

Ni vigumu kuamini ajali hii ambayo ilitokea usiku, ambapo baadhi ya watu walikua wameshalala. Ingawa uchunguzi bado haujaamua hali halisi ya tukio hili, mashahidi wanasema kuwa moto huo uliwashwa kwa makusudi. Polisi wa mji wa Lesbos imetangaza kwamba imewakamata watu wanane ambao wana uhusiano na ghasia hizo, huku ikiendelea kuwatafuta wengine kumi na nane.

Wakimbizi na wahamiaji wamekua wakirejea kwa mamia Jumanne hii katika kambi hii yenye msongamano mkubwa. Kama kila asubuhi, foleni ya watu imepigwa kwa ajili ya kupewa chakula katika eneo ambalo halikufikiwa na moto. Hata hivyo wafanyakazi wa manispaa wameanza kukarabati kambi hiyo.

Kwa mujibu wa mashahidi kadhaa wa tukio hilo, yote yaliianza saa mapema Jumatatu usiku. "Kulianza kusikika uvumi kwamba viongozi wa Ugiriki wamo mbioni kuanzisha upya zoezi la kuwahamishia wakimbi na wahamiaji wa kambi hiyo nchini Uturuki, " chanzo cha polisi kimesema. Wakati huo huo kulitokea mapigano baina ya makabila. Wakimbizi na wahamiaji kutoka Afrika na wale kutoka Pakistan na Afghanistan walikabiliana vikali. Hali ya taharuki ilikua ilitanda Jumatatu na ghafla motoulizuka katika sehemu tofauti katika kambi hiyo.

Wakimbizi wengi na wahamiaji wamekwama katika kambi hiyo baada ya makubaliano kati ya Umoja wa Ulaya na serikali ya Uturuki kuhusu kuwarejesha wakimbizi katika nchi wanakotoka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.