Pata taarifa kuu
UINGEREZA-UJERUMANI-IS-UGAIDI

Siri muhimu kuhusu wapiganaji wa IS waliosajiliwa yavuja

London na Berlin wanatahmini nyaraka zinazotaja majina ya watu wengi waliosajiliwa katika kundi la Islamic State (IS), taarifa ambayo imechukuliwa "pengine halisi" na polisi wa Ujerumani kuhusu wanajihadi kutoka Ujerumani, ingawa baadhi ya wataalam wametoa wito kwa tahadhari.

Picha ya propaganda iliyotolewa na vyombo vy habari vya  kijihadi vya Welayat Raqa,  inaonyesha wapiganaji wa kundi la Islamic State wakifanya maonyesho ya kijeshi katika mji wa Raqa, Juni 30, 2015, Syria.
Picha ya propaganda iliyotolewa na vyombo vy habari vya kijihadi vya Welayat Raqa, inaonyesha wapiganaji wa kundi la Islamic State wakifanya maonyesho ya kijeshi katika mji wa Raqa, Juni 30, 2015, Syria. AFP/WELAYAT RAQA/AFP/
Matangazo ya kibiashara

Jumatano usiku, runinga ya Uingereza ya Sky News ilitangaza kuwa ilipata nyaraka zenye majina ya watu 22,000 kutoka mataifa ya kigeni, wanaotaka kujiunga kwa minajili ya jihadi. Sky News ilisema kuwa nyaraka hizo ilizipata kutoka kwa mfuasi wa zamani wa kundi la IS aliejiita "Abu Hamed" ambaye aliziiba kutoka kwa mkuu wa polisi wa ndani wa kundi hilo la kijihadi kabla ya kulitoroka.

Nyaraka hizo, ni pamoja na fomu ziliojazwa majina ya watu kutoka nchi 55, zikiwa na majina yao, anwani au namba za simu. Pia wametakiwa kutoa "kiwango chao cha uelewa wa sharia" sheria ya Kiislamu, katiba yao na jina la mtu ambaye wanaweza kuwasiliana naye wakati wa matatizo, kama vile kifo.

Baadhi ya nyaraka hizo zina taarifa kuhusu wanajihadi mpaka sasa hawajatambuliwa ambao wanaendelea kuishi katika nchi za Ulaya Magharibi, Marekani, Canada, Kaskazini mwa Afrika na Mashariki ya Kati, kwa mujibu wa SKY NEWS.

Tovuti ya habari ilio karibu na upinzani nchini Syria ya ZAMAN AL WASL pia imesema kuwa ina milki nyaraka zote, zinazothibitisha mpango wa kundi la IS.

Msemaji wa serikali ya Uingereza amesema kuwa London mpaka sasa haijawa na taarifa kuhusu nyaraka hizo na inatathmini "jinsi tunaweza kutumia taarifa hizi kwa kupambana dhidi ya kundi la IS".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.