Pata taarifa kuu
SYRIA-IS-MAUAJI

Syria: kundi la IS ladai kuhusika na mashambulizi Damascus na Homs

Jumapili ya maafa nchini Syria, ambapo mfululizo wa mabomu ya kujitoa mhanga yatokea katika kitongoji cha Sayeda Zeinab, kusini mwa mji wa Damascus, na katikati mji wa Homs.

Askari wa Syria wakikagua eneo kulikotokea milipuko miwili ilioukumba mji wa Homs Jumapili Februari 21.
Askari wa Syria wakikagua eneo kulikotokea milipuko miwili ilioukumba mji wa Homs Jumapili Februari 21. REUTERS/SANA
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo yaligharimu maisha ya watu zaidi ya 140 na mamia kujeruhiwa.

Watu hamsini na tisa waliuawa katika mji wa Homs na angalau themanini karibu mji wa Damascus. Kundi la Islamic State limekiri kutekeleza mashambulii hayo. Hata hivyo kundi hili limeendelea kupoteza katika uwanja wa vita hasa katika mji wa Aleppo, kaskazini mwa nchi, dhidi ya majeshi ya serikali ya Syria.

Washambuliaji watatu labda wanne wa kujitoa mhanga,walitekeleza mashambulizi katika kitongoji cha Sayeda Zeinab, kusini mwa mji wa Damascus, ambapo kunapatikana kaburi la Zeinab, mjukuu wa Mtume Muhammad, anayeheshimiwa na Mashia.

Kulitokea kwanza shambulio la bomu lililokua limetegwa ndani ya gari karibu na hospitali ya Sadr, na kusababisha vifo vya watu wengi. Wakati watu walipoanza kuongezeka kwa kusaidia watu waliojeruhiwa, washambuliaji wawili au watatu wa kujitoa mhanga walilipua mikanda yao iliokua imejaa vilipuzi katikati ya umati wa watu. Mashambulizi hsyo yalitokea wakati wanafunzi walipokua wakitoka shule, hali ambayo inaeleza kuwa idadi kubwa ya wanafunzi ni miongoni mwa wahanga.

Katika mji wa Homs, wanajihadi waliamua kuendesha mashambulizi waati wanafunzi walipokua wakitoka katika madarasa. Tukio ni sawa na lile lililotokea katika mji wa Damascus: bomu lililotegwa ndani ya gari lilipuka katika njia panda, kwenye barabara ya mabasi ndgo za uchukuzi lkatika kitongoji cha wanakoishi watu wengi kutoka jamii ya Maalawi wa Zahraa. Mshambuliaji mwingine alijilipua katika ya umati wa watu.

Mashambulizi ya Homs na Sayeda Zeinab, yamesababisha nyumba nyingi ikiwa ni pamoja na duka na magari madogo kuharibika.

Wimbi hili la mashambulizi linatokea wakati kundi la Islamic State limeendelea kupoteza katika uwanja wa vita dhidi ya jeshi la Syria, mashariki mwa mji wa Aleppo, ambapo limepoteza katika masaa 48, wapiganaji hamsini. Wanajeshi wa serikali wamechukua zaidi ya vijiji 30 kutoka mikononi mwa kundi hili la IS, na sasa wanawanakaribia jimbo la Raqqa, ngome kuu ya kundi la Islamic State nchini Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.