Pata taarifa kuu
SYRIA-MISAADA-UN

Syria: msafara wa kwanza wa malori ya misaada waingia Mouadamiyat al-Sham

Msafara wa kwanza wa magari ya misaada umeingia Jumatano hii katika mji unaozingirwa na waasi wa al-Sham Mouadamiyat karibu na mji wa Damascus, kwa mujibu wa shirika la Msalaba Mwekundu.

Malori ya shirika la Msalaba Mwekundu yakiwa njiani kuondoka katika mji wa Damascus Februari 17, 2016 kwenda katika miji ya Madaya na Zabadani.
Malori ya shirika la Msalaba Mwekundu yakiwa njiani kuondoka katika mji wa Damascus Februari 17, 2016 kwenda katika miji ya Madaya na Zabadani. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Huu ni msaada wa kwanza wa kibinadamu tangu ufikiwe Mkataba wa mjini Munich, ambao uliamu kuwapatishia haraka msaada raia wanaokabiliwa na hali tete nchini Syria.

"Msafara ulianza kuingia katika mji wa Mouadamiyat al-Sham. Malori 35 yanayobeba magunia 8,800 ya unga, mgawo 4,400 wa chakula, pamoja na vyakula zaidi vya kuongeza nguvu muilini na madawa mbalimbali ikiwa ni pamoja na vifaa vya uzazi," afisa wa shirika la Msalaba Mwekundu, Mouhanad al-Assadi, ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Malori kadhaa ya misaada yamekua yakijiandaa kuingia Jumatano hii mchana katika miji inayozingirwa nchini Syria, ambapo hali ya kibinadamu imekuwa "tete"kwa mujibu wa Berlin.Msafara wa kwanza wa magari ya misaada umeingia Jumatano hii katika mji unaozingirwa na waasi wa al-Sham Mouadamiyat karibu na mji wa Damascus, kwa mujibu wa shirika la Msalaba Mwekundu.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Staffan de Mistura alitangaza Jumanne mjini Damascus kutumwa kwa malori hayo nchini Syri , akisema kwamba Damascus ina "wajibu" wa kuwezesha Umoja wa Mataifa kutoa misaada kwa raia, kauli iliyoikera serikali ya Syria.

Malori 35 ya misaada yamekua yameshawasili Jumatano hii alaasiri katika kituo cha ukaguzi cha al-Sham Mouadamiyat, mji unaodhibitiwa na waasi karibu na mji wa Damascus ambao unadhibitiwa na majeshi wa serikali, mwandishi wa shirika la habari la Ufaransa la AFP ameshuhudia.

Afisa wa shirika la Msalaba Mwekundu nchini Syria, Mouhanad al-Assadi, aliarifu mapema kwamba "magari 100 yanayobeba chakula, unga na madawa" yako njianikuelekea katika "katika maeneo yanayodhibitiwa".

Magari mengine 18 yameelekeakatika maeneo ya Foua na Kafraya, vijiji viwili vinavyokaliwa na Mashia katika jimbo la Idleb (kaskazini magharibi) na ambavyo vinadhibitiwa na waasi, kwa mujibu wa shirika la Msalaba Mwekundu.

Malori 50 yalikuwa pia yamepangwa kwenda katika miji ya Madaya na Zabadani, miji miwili pia jirani ya mji wa Damascus unaozingirwa namajeshi ya serikali.

Jumla ya watu 486,700 wako katika maeneo yanayodhibitiwa na milioni 4.6 katika maeneo ambayo ni vigumu kuingia, kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Msaada wa Kibinadamu (OCHA).

Kwa mujibu wa OCHA, maeneo mengine yanayodhibitiwa yatapokeaa misaada kama sehemu ya mji wa Deir Ezzor (Kaskazini-Mashariki) unaodhibitiwa na majeshi ya serikali na kuzingirwa na wanajihadi wa kundi la Islamic State (IS). Hadi sasa, msaada umekua ukitolewa na ndege za kijeshi za Syria au Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.