Pata taarifa kuu
IRAN-SAUDI-SYRIA-VITA

Iran yaonya dhidi ya kupelekwa kwa askari wa Saudi Arabia Syria

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Zarif, ameonya Jumanne hii kuwa kupelekwa kwa askari kutoka Saudi Arabia nchini Syria itakua ni kukiuka "sheria za kimataifa" na kudai kwamba Riyadh inapaswa kusitisha mashambulizi yake nchini Yemen.

Waziri wa mambo ya Nje wa Iran Mohammad Zarif, katika mkutano na waandishi wa habari katika Bunge la Ulaya mjini Brussels, Februari 15, 2016.
Waziri wa mambo ya Nje wa Iran Mohammad Zarif, katika mkutano na waandishi wa habari katika Bunge la Ulaya mjini Brussels, Februari 15, 2016. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

"Wale ambao wanaendesha operesheni za kijeshi nchini Syria bila idhini ya serikali ya Syria wanakiuka sheria za kimataifa", amesema Bw Zarif katika mkutano na waandishi wa habari katika Bunge la Ulaya mjini Brussels. Saudi Arabia inasaidia utawala wa Bashar al-Assad.

Bw Zarif alipoulizwa kuhusu tangazo lililotolewa na Saudi Arabia kwamba inaweza kupeleka majeshi ya ardhini ambayo yatashirikiana na majeshi ya muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani dhidi ya kundi la Islamic State.

"Tunaamini kwamba jaribio lolote la kuhusisha nchi nyingine kwa idadi kubwa katika vita katika Ukanda huu ni hatari", Mohammad Zarifa amesema katika mahojiano akiwa pamoja na mwenzake wa Ubelgiji Didier Reynders

"Nadhani kila mmoja anapaswa kujaribu kutafuta ufumbuzi wa amani, si kujenga hatari zaidi na uhasama katika ukanda huu", ameongeza Bw Zarif, akishtumu Saudi Arabia kwa kutumia "hoja ya kisiasa" ili kuvutia upande wa tatu katika mgogoro huo.

Iran, ambayo ilimtuma maelfu ya "washauri wa kijeshi" nchini Syria, pia inasaidia serikali ya Damascus kupitia mshirika wake wa Lebanon, ambaye ni chama cha Hezbollah, na hasa wa wanamgambo wa Kishia wa Iraq.

"Iran haina askari katika ardhi ya Syria. Tuna washauri wa kijeshi nchini Syria, kama katika maeneo mengine, kwa mwaliko wa serikali", Bw Zarif ameelezea Bunge la Ulaya.

jaribio la mazungumzo kati ya wadau wote nchini Syria chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa limemeshindikana mjini Geneva mwanzoni mwa mwezi Februari na baada ya uzinduzi wa mashambulizi ya serikali ya Syria, yanayoaungwa mkono na mashambulizi makali ya Urusi dhidi ya mji wa Aleppo, kaskazini mwa Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.