Pata taarifa kuu
SYRIA-USALAMA-MASHAMBULIZI

Syria: watu 57 wauawa katika mashambulizi Homs

Idadi ya watu waliouawa katika mfululizo wa mashambulizi yaliotokea katika mji wa Homs, nchini Syria imeongezeka na kufikia kwa sasa 57. Idadi hiyo ni kubwa katika katika mashambulizi kama haya tangu mwezi Oktoba mwaka 2014 katika mji huo wa tatu nchini Syria.

Eneo lkulikotokea mashambulizi mawili ya mabomu katika kitongoji cha Homs, Februari 21, 2016.
Eneo lkulikotokea mashambulizi mawili ya mabomu katika kitongoji cha Homs, Februari 21, 2016. STRINGER/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Shirika la Haki za Binadamu (OSDH) ambalo limetoa idadi hiyo mpya, hii ni idadi kubwa tangu kutokea kwa mashambulizi mawili dhidi ya shule ya kata ya Akrama katika mji wa Homs mwezi Oktoba mwaka 2014, na kuua watu wasiopungua 55 wakiwemo watoto 49.

Moja ya mashambulizi hayo limetokea katika eneo linalokaliwa na watu wengi kutoka Jamii ya Mashia Kusini mwa mji wa Damas, kwa mujibu wa runinga ya serikali na shirika lisilo la kiserikali.

Awali runinga ya serikali imearifu kwamba watu 30 wameuawa katika mashambulizi matatu ya bomu yaliokua yametegwa ndani ya gari na mengine mawili yaliotekelezwa na washambuliaji wa kujitoa mhanga.

Mwishoni mwa mwezi Januari, kwa uchache watu 70 waliuawa katika milipuko mitatu karibu na kaburi, mashambulizi yaliodaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State (IS).

Eneo la Sayeda Zeinab ni sehemu kubwa takatifu kwa watu kutoka jamii ya Mashia, ambapo kunapatikana kaburi la mjukuu wa kike wa Mtume Muhammad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.