Pata taarifa kuu
IRAQ-SHAMBULIZI-MAUAJI

Iraq: EI yakiri kuhusika na shambulizi kusini mwa Baghdad

Kundi la Islamic State (IS) limekiri kuhusika na shambulizi la kujitoa mhanga lillilowaua watu wasiopungua 47 Jumapili hii kusini mwa mji wa Baghdad, nchini Iraq.

Eneo la shambulizi la kujitoa mhanga mjini Baghdad, Mach 6, 2016.
Eneo la shambulizi la kujitoa mhanga mjini Baghdad, Mach 6, 2016. AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliorushwa hewani kwenye mitandao ya kijamii, kundi la Islamic State (IS) limesema kwamba mshambuliaji wa kujitoa mhanga, anayejulikana kama Abu Islam al-Ansari, amelipua lori la mafuta lililokua limetegwa bomu karibu na eneo la kukagua magari nje na mji mkuu mkuu wa Baghdad karibu na mji wa Hilla.

"Rafida "(neno linalotumiwa kwa kuwaita Waislamu wa kutoka jamii ya Mahia) lwanapaswa kuelewa kwamba vita ndiyo tu vinaanza na mbaya zaidi bado inakuja," taarifa hiyo imeeleza.

IS, kundi la Kisuni lenye msimamo mkali, limezidisha mashambulizi dhidi ya Mashia linalowachukulia kama wazushi.

Shambulizi hili lililowaua watu wasiopungua 47 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 72 waliojeruhiwa ni shambulizi baya la bomu kutegwa ndani kuwahi kutokea tangu mwanzoni mwa mwaka huu nchini Iraq.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.