Pata taarifa kuu
UGANDA-UFARANSA-UKAGUZI-WAHAMIAJI

Ubelgiji yakabiliana na ongezeko la wahamiaji

Polisi wa Ubelgiji wamekua wakiendelea Jumatano hii na zoezi la ukaguzi wa magari kutoka Ufaransa katika eneo la mpakani la La Panne (kaskazini magharibi), ili kukabiliana na uwezekano wa ongezeko la wahamiaji wanaotokea eneo la "Jungle" katika jimbo la Calais.

Polisi ya Ubeliji yafanya ukaguzi katika gari ndogo katika eneo la Adinkerke kwenye mpaka na Ufaransa, Februari 24, 2016.
Polisi ya Ubeliji yafanya ukaguzi katika gari ndogo katika eneo la Adinkerke kwenye mpaka na Ufaransa, Februari 24, 2016. AFP/Belga/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwenye barabara kuu "Duinkerkekeiweg" inayounganisha mji wa Ufaransa na ule wa Dunkirk, kilomita zaidi ya kumi upande wa magharibi, nchini Ubelgiji, magari madogo mawili ya polisi yameegesha kando ya barabara.

Askari watatu wamekua wakikagua magari, magari madogo na malori, na wamekua wakiendesha haraka zoezi la ukaguzi kwenye eneo la mizigo kabla ya kuyaruhusu kuendelea na safari nchini Ubelgiji.

Kilomita moja mbali na eneo hilo, kwenye barabara nyingine, hali hiyo hiyo imeshuhudiwa mara kwa mara. Polisi wawili wakiwa na farasi wamekua wakipiga doria ya nenda rudi kati ya vituo vya wili vya ukaguzi.

"Ni kuwahakikishia tu watu kile kinachoendelea, si kitu kingine. Wahamiaji wanaotaka kupita, hawatowakataza," amebaini Dominique, maarufu "Bouba" fundi, mwenye umri wa miaka 55, mzaliwa wa Touquet (Ufaransa), ambaye alingia Ubelgiji "kununuatumbaku" nchini Ubelgiji.

Ubelgiji ilitangaza Jumanne wiki hii kuwa imerejesha ukaguzi wa muda kwenye mpaka wake na Ufaransa ili kukabiliana na ongezeko la wahamiaji wanaotokea eneo la 'Jungle" katika jimbo la Calais, kambi kubwa inayopatikana kilomita kumi na tano na eneo la mpakani nchini Ufaransa.

Hayo yakijri suala la wahamiaji au wakimbizi limekua tetea katika eneo la Idomeni kwenye mpaka wa Ugiriki na Makedonia, ambapo wakimbizi au wahamiaji wameambiwa mtu asiekuwa na pasi ya usafiri hana haki ya kuingia Ugiriki. Ugiriki na nchi jirani zinakabiliana na ongezeko la wahamiaji wanaoingia katika mataifa hayo. Hali hii inashuhudiwa katika nchini za Makedonia, Serbia, Croatia, Slovenia na Austria. Hivi karibuni baadhi ya wakimbizi kutoka Syria wamefukuzwa nchini Ugiriki. Hali hii imeendelea kushuhudiwa katika baadhi ya nchi za Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.