Pata taarifa kuu
AUSTRIA-UJERUMANI-WAKIMBIZI-USALAMA

Austria kujenga uzio ili kudhibiti wimbi la wahamiaji

Serikali ya Austria imetangaza Jumatano Oktoba 28 nia yake ya kujenga uzio katika mpaka na Slovenia. Uamzi huu umechukuliwa ili kuweza kudhibiti wimbi la wahamiaji ambao wanawasili kwa wingi wakipitia kwa kile kinachoitwa " barabara ya nchi za Balkan". Katika hali yoyote, imesema serikali ya Vienna, siyo kufunga mpaka.

Austria tayari imeweka vizuizi vya chuma kwenye mpaka wake na Slovenia ili kukabiliana nawimbi la wahamiaji.
Austria tayari imeweka vizuizi vya chuma kwenye mpaka wake na Slovenia ili kukabiliana nawimbi la wahamiaji. REUTERS/Srdjan Zivulovic
Matangazo ya kibiashara

Katika mpaka wa Šentilj, maelfu ya wahamiaji wamekua wakisubiri kupita nchini Austria. Mara kwa mara treni au basi huwabeba wakimbizi wapya kutoka kusini mwa Slovenia, mwandishi wa RFI katika Ukanda huo, Laurent Geslin amearifu. Wengi hawajui jina la nchi ambayo wanajiandalia kuondoka na kuuliza kama nchi inayofuata ni Austria.

Wengi wao wanataka kwenda Ujerumani na hawajui kuwa Vienna kwa upande inatishia kuifunga mipaka yake. Kwa wao, swali ni kujuai wataendelea kusubiri hadi lini. Kama uwezo wa mapokezi katika vituo vyake tayari umejaa, Austria imechukua uamzi wa kupiga marufu mabasi kuendelea kuwatafuta wakimbizi. Wakimbizi hao wanasubiri katika mistari kati ya nchi hizo mbili, nyuma ya vizuizi vya chuma viliyowekwa na polisi ya Austria. Waliondoka Syria siku 10 zilizopita au wiki mbili na kujua kwamba wanakaribia kufikia lengo. Lakini swali moja linawakera: watapata hifadhi kweli?

Tangazo la kufungwa kwa mpaka wa Austria lazua utata

Baada ya kuzidiwa na wimbi la wahamiaji, Austria imetangaza Jumatano nia yake ya kujenga kizuizi katika mpaka wake na Slovenia, baada ya kukanusha tangu siku kadhaa uvumi kuhusu mpango huo. Katika taarifa zao, viongozi wa Austria wameepuka kusitisha ujenzi wa uzio huo, mwandishi wa RFI katika mji wa Vienna, Christian Fillitz. Kwa mujibu wa Kansela Faymann mpaka sasa mtetezi wa sera za Kiliberali za mapokezi kama Ujerumani, uzio pia una mlango, na inabidi kudhibiti mtiririko wa wahamiaji. Hakuna haja ya kufunga mpaka.

Ujerumani yaikosoa wazi Austria

Tangazo hilo linatolewa wakati ambapo mvutano kati ya Berlin na Vienna umeanza kujitokeza. Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Thomas de Maiziere amewakosoa wazi majirani zake, mwandishi wetu katika mji wa Berlin, Pascal Thibaut amearifu. Anawatuhumu kutaka kuwafukuza wakimbizi wengi waliopo katika ardhi zao. Thomas de Maiziere anaituhumu Austria kuwaingiza wahamiaji usiku nchini Ujerumani, bila hata hivyo kuwafahamisha. Jumanne, Oktoba 27, zaidi yawakimbizi 7,000 waliwasili katika mji wa Bavaria, mkoa wa mpakani na Austria, kwa jumla ya 9000 walioorodheshwa nchini Ujerumani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.