Pata taarifa kuu
UJERUMANI-WAKIMBIZI-MAPOKEZI

Katika mkutano wa CDU, Merkel ahadi kupunguza uhamiaji

Jumatatu wiki hii, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametetea kwa nguvu sera yake kwa wakimbizi wakati wa mkutano wa chama chake cha Conservative, CDU, huku akiwaambia wapinzani wake kwamba yuko mbioni kupunguza kwa"kiasi kikubwa" ongezeko la wahamiaji.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel mbele ya wajumbe wa chama chake cha Conservative cha CDU, amesema yuko tayari kupunguza wimbi la wakimbizi nchini mwake.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel mbele ya wajumbe wa chama chake cha Conservative cha CDU, amesema yuko tayari kupunguza wimbi la wakimbizi nchini mwake. REUTERS/Kai Pfaffenbach
Matangazo ya kibiashara

Hata kama aliteuliwa "Mtu muhimu katika Mwaka 2015" na magazeti ya Time pamoja na Financial Times kwa mtizamo wake wa mgogoro wa wahamiaji, Kansela Angela Merkel kwa sasa anakabiliwa katika nchi yake na upinzani mkubwa kwa sera yake ya mapokezi, ingawa, tangu mwanzoni mwa mwaka huu, Ujerumani imepokea milioni moja ya wahamiaji wapya.

Katika hotuba yake mbele ya wajumbe wa chama cha CDU, Merkel ametoa ripoti ya mwaka mmoja peke ambapo Ujerumani ilisimama dhidi ya Urusi katika mgogoro wa Ukraine, ilitoa na fasi kwa makubaliano yalioruhusu Ugiriki kukubaliwa kubaki katika kundi la nchi zinazotumia sarafu ya Euro, na kuwapokea mamia ya maelfu ya wakimbizi waliokimbia vita na kunyimwa haki Mashariki ya Kati.

Uamuzi wa kuwapokea wakimbizi wanaokimbia vita na kunyimwa haki Mashariki ya Kati uliochukuliwa mwezi Agosti ulionyesha "umuhimu wa binadamu", Merkel amesema, huku akiahidi kupunguza wimbi la wakimbizi nchini mwake.

"Tunataka na tuko mbioni kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya wakimbizi", Angela Merkel amesema, huku akipigiwa makofi katika mkutano huo wa chama, uliofanyika katika mji wa Karlsruhe, katika eneo la Baden-Württemberg ambapo kutafanyika uchaguzi wa mikoa mwezi Machi.

Jumapili mwishoni mwa juma lililopita, Merkel alisema kwenye runinga ya taifa ya ARD kuwa yuko mbioni kupunguza wimbi la wahamiaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.