Pata taarifa kuu

Ndege ya kijeshi ya Urusi yaanguka ikiwa na watu 15

Ndege ya kijeshi ya Urusi iliyokuwa imebeba watu 15 imeanguka siku ya Jumanne wakati injini yake moja "ilipowaka moto" katika eneo la Ivanovo, kaskazini mashariki mwa Moscow, Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema.

Ajali zinazohusisha ndege za kijeshi zinazokumbwa na matatizo ya kiufundi hutokea mara kwa mara nchini Urusi.
Ajali zinazohusisha ndege za kijeshi zinazokumbwa na matatizo ya kiufundi hutokea mara kwa mara nchini Urusi. AP - Dmitri Lovetsky
Matangazo ya kibiashara

Mapema alasiri, "ndege ya usafiri ya kijeshi ya Il-76 imeanguka katika eneo la Ivanovo wakati ikipaa" ikiwa na "wafanyakazi wanane na abiria saba," Wizara ya Ulinzi imesema, ikinukuliwa na mashirika ya habari ya Urusi. Kulingana na habari za awali, ajali hiyo "ilitokana na moto kwene injini moja wakati ndge hiyo ilipokuwa ikipaa," wizara hiyo imeongeza.

Video zilizorushwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha ndege ikiwa na moja ya mbawa zake ikionekana kuwaka moto.

Ajali zinazohusisha ndege za kijeshi zinazokumbwa na matatizo ya kiufundi hutokea mara kwa mara nchini Urusi. Lakini nchi hiyo pia imepata majanga kadhaa ya anga yanayohusishwa na shambulio lake dhidi ya Ukraine, ambalo lilianza Februari 2022.

Mwishoni mwa mwezi wa Januari, Urusi iliishutumu Kyiv kwa kudungua ndege ya Il-76 katika eneo linalopakana na Ukraine, na kuwauwa watu wote waliokuwa ndani yake, ikiwa ni pamoja na wafungwa 65 wa Ukraine, kulingana na Moscow.

Kwa sasa hakuna dalili kwamba ajali ya siku ya Jumanne, iliyotokea mamia ya kilomita kutoka mpaka wa Ukraine, inahusishwa na mashambulizi ya Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.