Pata taarifa kuu

Hungary: Rais Katalin Novak ajiuzulu baada ya kutoa msamaha wenye utata

Rais wa Hungary Katalin Novak ametangaza kujiuzulu Jumamosi Februari 10 baada ya hasira iliyosababishwa katika nchi hiyo ya Ulaya ya kati kwa uamuzi wake wa kumsamehe mfungwa aliyehusika katika kesi ya uhalifu wa watoto.

Katalin Novak (hapa Aprili 2023) amekiri "kosa".
Katalin Novak (hapa Aprili 2023) amekiri "kosa". AP - Andrew Medichini
Matangazo ya kibiashara

 

Rais Katalin Novak, aliye karibu na Viktor Orban, amejiuzulu siku ya Jumamosi baada ya hasira iliyosababishwa na uamuzi wake wa kumsamehe mfungwa aliyehusika katika kesi ya uhalifu wa watoto.

“Ninajiuzulu kwenye wadhifa wangu,” ametangaza wakati wa hotuba yake rasmi rafiki huyu wa karibu wa Waziri Mkuu Viktor Orban, akikiri kuwa amefanya “kosa.” Mnamo mwezi Machi 2022, alikua mwanamke wa kwanza kuchukua wadhifa huu wa heshima.

Karibu wakati huo huo, Judit Varga, mshirika mwingine wa Waziri Mkuu, ametangaza "kuachia ngazi kwenye wadhifa wake" kwa kutoa idhini yake kama Waziri wa Sheria - wadhifa ambao alijiuzulu msimu huu wa joto ili kuongoza kampeni ya Ulaya. Hali ambayo bado haikufikirika siku chache zilizopita.

Mzozo huo ulichochewa na msamaha uliotolewa mwezi Aprili 2023, wakati wa ziara ya kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis huko Budapest, kwa naibu mkurugenzi wa zamani wa Jumba la kulelea watoto, aliyehukumiwa mwaka 2022 kifungo cha zaidi ya miaka mitatu jela kwa kuficha vitendo vya mkuu wake.

Tangu kufichuliwa na tovuti ya uchunguzi 444 wiki iliyopita ya uamuzi huu, upinzani umetoa wito wa kuondoka kwa wanawake hao wawili na hasira imekuwa ikiongezeka nchini. Siku ya Ijumaa jioni waandamanaji walikusanyika mbele ya ikulu ya rais na watatu kati ya washauri wa rais walijiuzulu kwenye nyadhifa zao.

Kurudi nyumbani haraka

Akikabiliwa na kashfa hiyo, Katalin Novak, ambaye alikuwa Qatar kuhudhuria mechi kati ya Hungary na Kazakhstan kwenye Mashindano ya Dunia ya Polo ya Maji, aliharakisha kurejea Budapest.

Mara tu ndege yake ilipotua, alitangaza kwamba anajiuzul kwenye wadhifa wake, akikiri kuwa amefanya "kosa". "Msamaha uliotolewa na kukosekana kwa maelezo kunaweza kuibua mashaka kuhusu kutostahimili katika masuala ya watoto. Lakini hakuna shaka juu ya suala hili,” alisisitiza meneja huyo mwenye umri wa miaka 46, kabla ya kuwasilisha “samahani” zake kwa wale ambao huenda amewaumiza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.