Rais wa Hungary Katalin Novak anazuru Tanazania
Nairobi – Rais wa Hungary Katalin Novak amewasili nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku nne, ziara inayolenga kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.
Imechapishwa:
Rais Novak, Rais wa kwanza mwanamke nchini humo anatembelea Tanzania kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kibiashara Uhusiano uliodorora, tangu kuasisiwa kwake miaka 1980.
Tanzania na Hungary zimekuwa zikishirikiana katika sekta ya elimu,ambapo nchi ya Hungary imekuwa ikiwafadhili wanafunzi kwenda kusoma elimu ya juu katika ngazi ya shahada ya kwanza, Uzamili na Uzamivu.
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akimpokea Rais wa Jamhuri ya Hungary Mhe. Katalin Novàk Ikulu jijini Dar es Salaam pic.twitter.com/qi6luNJFIW
— ikulu_Tanzania (@ikulumawasliano) July 18, 2023
Wanafunzi hao kutoka Tanzania wamekua wakifadhiliwa katika Masomo ya Sayansi na Teknolojia,Uhandisi, Mawasiliano, Hisabati miongoni mwa mengine.
Kwa Mujibu wa Shirika la Fedha Duniani IMF, nchi ya Hungary ni ya 57 Duniani kwa ukuaji kiuchumi kati ya nchi 188 na kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi uliomarika Zaidi barani Ulaya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni wake Rais wa Hungary Mhe. Katalin Novák mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe18 Julai, 2023. pic.twitter.com/uXL7vj8uvx
— ikulu_Tanzania (@ikulumawasliano) July 18, 2023
Ziara hiyo inatarajiwa kutamatika Julai 20 mwaka huu mara baada ya kuzungumza na mwenyeji wake Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.