Pata taarifa kuu

Ukraine: Mkuu wa Majeshi Valery Zalouzhny afukuzwa kazi

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametangaza siku ya Alhamisi Februari 8 kwamba amemteua Kamanda Mkuu wa Jeshi, Oleksandr Syrsky, Mkuu mpya wa Jeshi la Ukraine kuchukua nafasi ya Valery Zalouzhny, na kumaliza siku kadhaa za uvumi juu ya mustakabali wa jeshi.

Katika picha hii iliyotolewa na ofisi ya vyombo vya habari vya rais wa Ukraine, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, kushoto, akipeana mkono na Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Wanajeshi wa Ukraine Valery Zaluzhny wakati wa mkutano wao mjini Kyiv, Alhamisi, Februari 8, 2024.
Katika picha hii iliyotolewa na ofisi ya vyombo vya habari vya rais wa Ukraine, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, kushoto, akipeana mkono na Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Wanajeshi wa Ukraine Valery Zaluzhny wakati wa mkutano wao mjini Kyiv, Alhamisi, Februari 8, 2024. AP
Matangazo ya kibiashara

Valery Zalouzhny, 50, aliteuliwa mnamo mwezi wa Julai 2021. Mafanikio yake dhidi ya jeshi la Urusi yamemfanya asifiwe na raia wenzake na kuheshimiwa na washirika wake wa Magharibi. Lakini mvutano ulikuwa ukiongezeka kwa miezi kadhaa kati ya rais na yeye. Ni mabadiliko muhimu zaidi ndani ya jeshi tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi.

Β 

Kiongozi huyo wa Ukraine amebaini kuwa wakati umefika wa kufanya mabadiliko katika uongozi wa jeshi, huku vita dhidi ya Urusi vikiingia mwaka wa tatu. Kupitia ujumbe wa Telegram, Volodymyr Zelensky amesema kwamba alizungumza wakati wa mchana na Valery Zalouzhny, ambaye alimwomba "kusalia katika timu yake", wakati jenerali huyo anachukuliwa na watu wengi wa Ukraine kama shujaa wa kitaifa wa kusimamia operesheni za jeshi tangu uvamizi ulioanzishwa na Urusi mnamo Februari 24, 2022.

"Tulijadili urekebishaji ambao jeshi linahitaji. Pia tulijadili utambulisho wa wale ambao wanaweza kujumuishwa katika kamandi mpya ya jeshi. Wakati wa kulifanyia upya urekebishaji jeshi sasa umefika,” rais wa Ukraine ameandika.

Katika taarifa tofauti, Waziri wa Ulinzi Roustem Umerov amebainisha kuwa uamuzi ulifanywa wa kufanya mabadiliko katika uongozi wa jeshi.

Valery Zalouzhny amesema kwa upande wake kwamba alikuwa na "mazungumzo muhimu" na Volodymyr Zelensky wakati ambao walikubali kurekebisha mikakati kwenye viwanja vya vita.

Β 

"Misheni za 2022 zilikuwa tofauti na misheni za 2024. Kwa hivyo, kila mtu lazima abadilike na kuzoea hali halisi mpya. Ili kushinda pamoja,” alisema kupitia ujumbe wa Telegram.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.