Pata taarifa kuu

Ufaransa: Vyama vingi vya wafanyakazi wa kilimo vinataka kusitishwa kwa vizuizi

Vyama vingi vya wafanyakazi wa kilimo nchini Ufaransa vimetoa wito siku ya Alhamisi, Februari 1, 2024, kusimamisha vizuizi, baada ya msururu wa matangazo kutoka kwa Waziri Mkuu Gabriel Attal kwa kuiunga mkono sekta hiyo iliyoko kwenye mzozo.

Mnamo Januari 30, 2024, matrekta yakifunga barabara kuu ya Longvilliers karibu na Paris.
Mnamo Januari 30, 2024, matrekta yakifunga barabara kuu ya Longvilliers karibu na Paris. REUTERS - ABDUL SABOOR
Matangazo ya kibiashara

 

"Kwa kuzingatia kila kitu kilichotangazwa [...], tunahitaji kubadilisha njia zetu za utekelezaji na kwa hiyo tunatoa wito kwa mitandao yetu [...] kusitisha vizuizi na kuingia katika aina mpya ya uhamasishaji", ametangaza mkuu wa Wakulima Vijana, Arnaud Gaillot, pamoja na mwenyekiti wa muungano wenye nguvu wa kilimo FNSEA Arnaud Rousseau, ambao wamekaribisha "maendeleo yanayoonekana".

Vyama vya wafanyakazi vinaweka masharti kadhaa ya kutoanzisha tena maandamano: "matokeo ya kwanza" kwenye Maonyesho ya Kilimo (Februari 24 - Machi 3) kisha kupitishwa kwa sheria ya mwelekeo wa kilimo na siku zijazo pamoja na hatua za Ulaya tu kati ya sasa na mwezi Juni. "Ikiwa pointi hizi hazitafikiwa kufikia hadi mwezi Juni, hatutasita kuingia tena mitaani," amesema Arnaud Gaillot. Maafisa hao wawili wameomba waraka wa maneneo mafupii unaoweka kwa maandishi matangazo yote ya serikali.

Kabla ya Maonyesho ya Kilimo, "tuna wiki mbili kuona ikiwa yote haya ni mbaya, ni ya kuaminika, yako sawa" ameongeza Arnaud Rousseau. Mkuu wa FNSEA kwa ujumla amekaribisha “usikizi” wa Waziri Mkuu “kujaribu kuelewa masuala yetu ni nini, kutupokea, kuzungumza nasi, kujadili na hatimaye kutangaza hatua za dharura”.

"Wakati huo huo, tunatilia shaka uziwi wa Uropa," aliongeza Arnaud Rousseau, akimaanisha "kutokuelewana kunakua kati ya muundo wa kiteknolojia uliozungukwa na ukuta katika ofisi zake huko Brussels na ukweli wa kile tunachopata kwenye shamba letu" . Mara tu baada ya taarifa hizi, Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen alitangaza pendekezo la "kupunguza mzigo wa kiutawala" unaowaelemea wakulima, ili kujibu hasira ya sekta hii. "Tutafanya kazi na rais wa Ubelgiji [wa Baraza la EU] kwa pendekezo ambalo tutawasilisha [...] ili kupunguza mzigo wa kiutawala" wa Sera ya Pamoja ya Kilimo, ametangaza afisa wa Ujerumani mwishoni mwa mkutano wa Umoja wa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.