Pata taarifa kuu
UCHUNGUZI-USALAMA

Ajali ya ndege iliyobeba wafungwa wa Ukraine: Putin ashtumu 'kombora la Marekani'

Ndege ya kijeshi ya Il-76 iliyoanguka wiki iliyopita nchini Urusi ikiwa na, kwa mujibu wa Moscow, wafungwa wa Ukraine waliokuwa ndani ya ndege hiyo, ilitunguliwa "kwa uhakika" kwa kutumia "mfumo wa kombora la Patriot la Marekani", amesema Rais Vladimir Putin, siku ya Jumatano, Januari 31.

"Tunadai na kusisitiza kwamba kuwe na uchunguzi wa kimataifa," Vladimir Putin amesema siku ya Jumatano.
"Tunadai na kusisitiza kwamba kuwe na uchunguzi wa kimataifa," Vladimir Putin amesema siku ya Jumatano. via REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

 

"Ndege ilidunguliwa, hii tayari ilifanywa kwa uhakika, na mfumo wa kombora la Patriot la Marekani" lililorushwa kutoka "eneo linalodhibitiwa na vikosi vya Ukraine," amesema Vladimir Putin katika hafla iliyoandaliwa huko Moscow.

"Uhakika wa kwamba waliiangusha ndege walimokuwa wanajeshi wao unaturuhusu kudhani kwamba walifanya hivyo kwa bahati mbaya. Lakini bado ni uhalifu," ameongeza, akibaini kwamba Kiev ilitaka "kuchokoza" Urusi "kujibu."

Maswali yameendelea kuwa mendi wiki moja baada ya kuanguka kwa ndege ya kijeshi ya Urusi karibu na mpaka na Ukraine.

Ukraine imeomba kufunguliwa kwa uchunguzi wa kimataifa

Urusi inahakikisha kwamba jeshi la Ukraine liliidungua ndege iliyokuwa na watu 74, ikiwa ni pamoja na, kulingana na Moscow, wafungwa 65 wa vita wa Ukraine ambao walikuwa wakienda kubadilishana. Lakini katika hatua hii, mamlaka ya Urusi haijatoa ushahidi unaothibitisha kwa uhakika kwamba wafungwa wa vita wa Ukraine walikuwepo katika ndege hii na kwamba Kyiv ilijua hilo, kama inavyodai Moscow.

Ukraine, kwa upande wake, haijazungumzia moja kwa moja kuhusika kwake na tukio hilo na imeelezea mashaka juu ya uwepo wa askari wake kwenye ndege hiyo.

Mamlaka ya Kyiv, hata hivyo, inabainisha kwamba kubadilishana kwa wafungwa kulipangwa siku ya ajali, na hatimaye zoezi hilo halikufanyika. Volodymyr Zelensky pia ametoa wito wa kufunguliwa kwa uchunguzi wa kimataifa.

"Tunadai na kusisitiza kwamba kuwe na uchunguzi wa kimataifa," Vladimir Putin amesema siku ya Jumatano.

Lakini "hakuna mashirika ya kimataifa yaliyo tayari kufanya hivyo," ameogeza.

Mapema siku ya Jumatano, Moscow na Kyiv walitangaza kuwa walibadilishana karibu wafungwa 200 wa vita kutoka kila upande, licha ya mvutano juu ya kuanguka kwa ndege ya kijeshi ya Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.