Pata taarifa kuu

Urusi: Watu 14 wauawa katika mashambulizi dhidi ya Belgorod

Moscow imeshutumu jeshi la Ukraine Jumamosi Desemba 30 kwa shambulio lililosababisha vifo vya watu kumi na wanne, wakiwemo watoto wawili, na 108 kujeruhiwa siku ya Jumamosi huko Belgorod, mji wa Urusi karibu na mpaka, siku moja baada ya mashambulizi makubwa yaliyoua watu 39 nchini Ukraine. Urusi imeomba mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Wazima moto wakizima gari lililokuwa likiungua kufuatia kile kinachoaminika kuwa ni shambulizi la makombora lililofanywa na vikosi vya Ukraine huko Belgorod, Urusi, Desemba 30, 2023.
Wazima moto wakizima gari lililokuwa likiungua kufuatia kile kinachoaminika kuwa ni shambulizi la makombora lililofanywa na vikosi vya Ukraine huko Belgorod, Urusi, Desemba 30, 2023. via REUTERS - RUSSIAN EMERGENCIES MINISTRY
Matangazo ya kibiashara

"Kulingana na habari za hivi punde, watu wazima 12 na watoto wawili wameuawa huko Belgorod," Wizara ya Hali ya Dharura ya Urusi imesema kwenye Telegraph, na kuongeza kuwa "watu 108, ikiwa ni pamoja na watoto kumi na tano, wamejeruhiwa."

Picha zilizochapishwa mtandaoni zinaonyesha magari yakiteketea kwa moto, majengo yenye madirisha yaliyovunjika.

Ukraine mara kwa mara hufanya mashambulizi nchini Urusi, hasa katika mikoa iliyo karibu na ardhi yake.

Wizara ya Ulinzi imehakikisha kwamba shambulio hili "halitabaki bila kuadhibiwa". Wakati huo huo Urusi inataka mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakutana Jumamosi saa tatu usiku saa za New York kujadili mashalbulizi ya Belgorod, ujumbe wa Urusi katika Umoja wa Mataifa umetangaza. "Leo (...) mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa utaitishwa na Urusi kuhusu mashambulizi ya Belgorod," ujumbe huo umesema kwenye mitandao ya kijamii. Taarifa hizo zimethibitishwa kwa shirika la habari la AFP na wajumbe wawili wa Baraza hilo.

Vikosi vya Urusi vimefanikiwa kuzuia makombora mawili na roketi nyingi zilizorushwa dhidi ya jiji hilo, ujumbe umeongeza, hali ambayo imeepusha vifo vingi. Hata hivyo, roketi kadhaa na mabaki ya makombora vimeangukia Belgorod, umeongeza.

Ukraine bado ilikuwa ikihesabu watu waliouawa siku ya Jumamosi, baada ya mashambulizi mkali siku moja kabla katika miji kadhaa, ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa Kyiv. Wimbi la mashambulizi, moja ya vurugu zaidi tangu kuanza kwa vita karibu miaka miwili iliyopita, yalilenga majengo, wodi ya wazazi na hata kituo cha biashara, lakini pia miundombinu ya viwanda na kijeshi. "Kwa sasa, kwa bahati mbaya watu 39 waliuawa" kote nchini, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alitangaza Jumamosi, akiongeza kuwa karibu watu mia moja wamejeruhiwa.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.