Pata taarifa kuu

Ukraine yapata msaada zaidi kutoka kwa Marekani kupambana na Urusi

Marekani imeidhinisha msaada mwingine wa kijeshi kwa Ukraine, wenye thamani ya Dola Milioni 250.

Jeshi la Ukraine
Jeshi la Ukraine © Evgeniy Maloletka / AP
Matangazo ya kibiashara

Huu ndio msaada wa hivi punde wa kijeshi, itakayosaidia Ukraine kupata vifaa vya kisasa, katika makabiliano dhidi ya jeshi la Urusi.

Huu ni msaada wa mwisho uliotolewa moja kwa moja kutoka Ikulu ya Marekani, kwenda kwa Ukraine, bila ya kupitia bunge la Congress.

Hatua hii inakuja baada ya Ukraine, kuonya kuwa vita vyake dhidi ya Urusi huenda vikayumba iwapo haitapata msaada wa haraka kutoka kwa washirika wake wakiongozwa na Marekani.

Mbali na Marekani, mwezi uliopita, Umoja wa Ulaya ulipitisha bajeti ya Euro Bilioni 50 kuisaidia Ukraine, lakini ikazuiwa na Hungary.

Wakati huu vita vikiendelea, Ukraine inasema ina upungufu wa Dola Bilioni 43 na hivyo inakabiliwa na changamoto ya kulipa mishahara ya wafanyakazi wa serikali.

Urusi imeapa kuendelea kupigana nchini Ukraine, hadi pale itakapopata ushindi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.