Urusi yatekeleza mashambulio mazito ya anga dhidi ya Ukraine
Nairobi – Urusi ilitekeleza mashambulio makubwa ya anga dhidi ya Ukraine siku ya Ijuma, mashambulio ambayo yamesababisha karibia vifo vya watu 30 na kuwajeruhi mamia ya wengine.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Haya ni mashambulio makubwa zaidi kuwahi tekelezwa na Urusi tangu ilipoivamia Ukraine karibia miaka miwili iliyopita.
Shule, hosipitali ya kina mama kujifungua na majengo ya makazi ni miongoni mwa maeneo yalioharibiwa.
Mashambulio hayo ambabyo kombora la Urusi lilipitia anga ya Poland yalizua shutuma za kimataifa, washirika wa Kyiv wakitoa ahadi mpya za msaada wa kijeshi kwa Ukraine, ambayo imekuwa ikipambana na mashambulio ya wanajeshi wa Urusi tangu mwishoni mwa Februari 2022.
Jeshi la Ukraine lilikadiria kuwa Urusi ilikuwa imerusha makombora 158 na ndege zisizo na rubani katika ardhi ya Kyiv, 114 kati ya hizo ziliharibiwa.
Umoja wa mataifa umelaani mashambulio hayo na na kutaka yakomeshwe mara moja.
Poland ilithibitisha kuwa kombora la Urusi lilipita katika anga yake.
Msaidizi wa rais wa rais wa Ukraine Andriy Yermak baada ya mashambulio hayo ameeleza kuwa nchi yake inahitaji msaada zaidi kuzuia kile ametaja kuwa ugaidi.
Війна з пологовими будинками, ліцеями, багатоповерхівками, ТЦ…
— Andriy Yermak (@AndriyYermak) December 29, 2023
Божевільні терористи. pic.twitter.com/aKSmDVx4Jo