Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: askari wasiopungua 16,000 watoweka

Wakazi wa miji kadhaa nchini Ukraine wanaomboleza vifo vya dugu zao siku ya Jumamoi baada ya mfululizo mkubwa wa mashambulizi ya Urusi kwa "idadi ya rekodi ya makombora", ambayo yalisababisha, kwa mujibu wa mamlaka ya Ukraine, angalau watu 30 kuuawa na zaidi ya 160 kujeruhiwa.

Watu hutembelea makaburi ya askari wa Ukraine kwenye hafla ya Siku ya Wanajeshi wa Ukraine, kwenye makaburi ya Lychakiv katika mji wa magharibi wa Ukraine wa Lviv mnamo Desemba 6, 2023.
Watu hutembelea makaburi ya askari wa Ukraine kwenye hafla ya Siku ya Wanajeshi wa Ukraine, kwenye makaburi ya Lychakiv katika mji wa magharibi wa Ukraine wa Lviv mnamo Desemba 6, 2023. AFP - YURIY DYACHYSHYN
Matangazo ya kibiashara

Wakazi wa miji ya Zaporizhia, Dnipro na Odessa wanaomboleza vifo vya ndugu zao. Kando ya mstari wa vita, mapigano yanaendelea. Wengi wa wanajeshi waliouawa wakiwa kazini sasa hawajulikani waliko. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ukraine anaongeza idadi ya watu 16,000 ambao mamlaka ya Ukaine haiwezi kutambua.

Wanaume na wanawake hawa huonekana katika "daftari la watu waliopotea katika mazingira ya kipekee", daftari linalosimamiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani. Akinukuliwa na vyombo vya habari vya Ukraine, Ihor Klymenko amesisitiza kwamba wizara yake ilikuwa inakabiliwa na tatizo kubwa: jinsi ya kulinganisha DNA ya miili ya askari iliyopatikana kwenye uwanja wa vita, na wale wa jamaa zao ambao waliondoka kuishi kaika nchi za kigeni.

Mwezi uliopita, mamlaka ya Ukraine ilitoa wito kwa raia wao nchini Poland na Ujerumani, nchi mbili zinazohifadhi idadi kubwa ya wakimbizi. Kwa wiki moja, Tume ya Kimataifa iliyoundwa kwa minajili ya watu waliotowea, kwa kushirikiana na polisi wa Ukraine, ilifanya kampeni ya kukusanya sampuli za DNA kutoka kwa familia za watu wa Ukraine. Sampuli 165 ziliweza kupatikana. Mbali na data ya maumbile, wanafamilia pia walitoa habari kuhusu wapendwa wao waliotoweka, hali ya kutoweka kwao au mahali walipoonekana mara ya mwisho.

Mwanzoni mwa mwezi wa Januari, kampeni kubwa zaidi itazinduliwa, na maeneo ya kukusanya DNA yamepangwa katika nchi kadhaa zinazohifadhi wakimbizi wa Ukraine: Ujerumani na Poland, lakini pia Jamhuri ya Czech na Uhispania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.