Pata taarifa kuu

Uingereza: Serikali yatafuta suluhu ya mahakama ya juu kuhusu wahamiaji

Serikali ya Uingereza, wiki ijayo inatarajiwa kuanza kuwashawishi majaji wa mahakama ya juu nchini humo, kubatilisha uamuzi wa mahakama kuu ambayo ilisema mpango wa Serikali kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda, umevunja sheria.

Mpango huo umekosolewa na mashirika ya kutetea haki za binadamu pamoja na umoja wa Mataifa
Mpango huo umekosolewa na mashirika ya kutetea haki za binadamu pamoja na umoja wa Mataifa © Henry Nicholls/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Katika kile ambacho kilitajwa kama pigo kwa waziri mkuu Rishi Sunak, ambaye aliahidi kuzuia boti zinazosafirisha wahamiaji, mahakama ya rufaa mwezi Juni ilidai kuwa mpango wa Serikali kuwahamisha wahamiaji zaidi ya elfu 4 kwenda Rwanda, haukubaliki kisheria.

Jumatatu ya wiki ijayo, mawakili wa Serikali watakuwa na jukumu moja tu, kuwashawishi majaji kuwa, hukumu ya awali haikustahili, huku wale wanaowawakilisha wahamiaji kutoka Syria, Iraq, Vietnam na Sudan, wakiwataka majaji kukazia hukumu ya awali.

Kwa waziri mkuu Sunak, kesi ya wiki ijayo ni ya kufa au kupona, kutokana na kuwa miongoni mwa ahadi zake tano kuu alizoingia nazo madarakani, moja ilikuwa ni kudhibiti wimbi la wahamiaji.

Mpango huu umekosolewa na mashirika ya kutetea haki za binadamu pamoja na umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.