Pata taarifa kuu

Uingereza :Kundi la mamluki wa Wagner ni kundi la kigaidi,litapigwa marufuku

Nairobi – Serikali ya Uingereza kupitia waziri wake wa mambo ya ndani Suella Braverman, imesema inampango wa kulipiga marufuku kundi la Mamluki wa Wagner kwa kile inachosema kuwa ni kundi la Kigaidi.

Uingereza yatishia kuwapiga marufuku wanajeshi wa Wagner kwa kile wanachosema ni kundi la Kigaidi kama vile AlQaida
Uingereza yatishia kuwapiga marufuku wanajeshi wa Wagner kwa kile wanachosema ni kundi la Kigaidi kama vile AlQaida © @Reuters
Matangazo ya kibiashara

Waziri huyo ameongeza kuwa kundi hilo lilikua likisababisha ghasia na hivyo ni tishio kwa usalama wa kimataifa.

"Kwa maneno rahisi, wao ni magaidi - na amri hii ya marufuku inaweka wazi hilo katika sheria za Uingereza."alisema Suella Braverman

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza Suella Braverman,atishia kupigwa marufuku kwa kundi la Wagner la Urusi
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza Suella Braverman,atishia kupigwa marufuku kwa kundi la Wagner la Urusi AP - Peter Byrne

Kundi hilo lilianzishwa mnamo mwaka wa  2014 na kumekuwepo na taarifa ya kundi hilo kuhusika katika mauaji na mateso yanayoshudiwa katika mataifa ya Afrika Magharibi kama Mali  na mataifa mengine kama  Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Vilevile Kulingana na taarifa ni kuwa mamluki hao wa Wagner walikuwa na mchango mkubwa katika uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.

Uhusiano wa kundi hilo na Urusi uliingia maji mwanzoni mwa mwaka huu baada ya kiongozi wao kupanga uasi dhidi ya viongozi wa kijeshi wa Urusi.Mpango ambao haukufanikiwa.

Agosti 26 mwaka huu  Rais wa Urusi Vladmir Putin alitoa wito kwa kundi hilo na wanakandarasi wengine wa kijeshi  wa kibinafsi wa Urusi kula kiapo chakulitii taifa lake.

Putin alizungumzia haya baada tuu ya ndege iliyokuwa imebeba kiongozi wa Wagner, Yevgeny Prigozhin kuanguka na baadae taarifa kuwekwa wazi kuwa kiongozi huyo amefariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.