Pata taarifa kuu

Mtu mmoja amefariki na wanne kujeruhiwa baada ya daraja kuporomoka magharibi mwa Ugiriki

Mtu mmoja amefariki na wanne kujeruhiwa baada ya sehemu ya daraja kuporomoka kwa sababu zisizojulikana siku ya Jumapili huko Patras, magharibi mwa Ugiriki, polisi wa Ugiriki na vyombo vya habari wamesema.

Ugiriki inaendelea kukumbwa na majanga mbalimbali.
Ugiriki inaendelea kukumbwa na majanga mbalimbali. © AFP / ANGELOS TZORTZINIS
Matangazo ya kibiashara

Sehemu ya daraja ambalo ujenzi wake unaendelea liliporomoka siku ya Jumapili magharibi mwa Ugiriki. Mtu mmoja amefariki na wanne wamejeruhiwa katika mkasa huu, kwa sababu ambayo bado haijulikani, Jumapili hii huko Patras, imetangaza polisi ya Ugiriki na vyombo vya habari.

"Tunathibitisha kifo cha mtu mmoja," msemaji wa polisi ameliambia shirika la AFP. Shirika la habari la ANA na shirika la utangazaji la umma ERT, yakinukuu huduma za ambulensi, yamesema kuna majeruhi wanne, ambao wamehamishiwa katika hospitali mbili za jiji.

Matatizo ya uthabiti?

Operesheni kubwa ya uokoaji inaendelea na wazima moto na gari la wagonjwa kwenye eneo la tukio. Sababu za kudondoka kwa sehemu ya daraja hilo hazijajulikana katika hatua hii. daraja hili liko kwenye barabara inayounganisha bandari ya Patras, katika rasi ya Peloponnese (kusini-magharibi), hadi Athens.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Efthymis Lekkas, rais wa mamlaka ya kukabiliana na matetemeko ya ardhi, OASP, ambaye amenukuliwa na kituo cha ERT, daraja hilo lilikuwa na matatizo ya uthabiti ambayo yanajulikana kwa mamlaka. Kazi ya kukarabati daraja hili ilianza mnamo mwak 2021 kwa gharama ya zaidi ya euro milioni sita, kulingana na ERT.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.